Serikali yalaani mama kuzaa amesimama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yalaani mama kuzaa amesimama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Baada ya wabunge kuingilia kati kashfa ya mama kujifungua akiwa amesimama katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Serikali imetangaza kuchukua hatua kali kwa watu waliohusika na uzembe huo.

  Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana akiwa mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema Serikali inalaani tukio hilo, ambapo Wizara yake itawasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kuanza kazi ya uchunguzi mara moja.

  Kauli hiyo ya Serikali imekuja siku chache baada ya wabunge wanawake kutoa tamko la kulifikisha suala hilo kwenye vikao vya bunge, endapo Wizara husika haijachukua hatua kwa kuwafukuza kazi pamoja na kuwashtaki wauguzi waliosababisha mwanamke huyo Kuluthum Abdallah (35) kujifungua akiwa amelazimishwa kusimama.

  Kwenye tukio hilo lililotokea Aprili 18, mwaka huu majira ya saa 11.30 jioni, Kuluthum alilazimishwa na mmoja wa wauguzi (Jina lake halijafahamika) kusimama hadi alipojifungua mtoto wakati alipofika kwenye hospitali hiyo kupatiwa huduma ya uzazi.

  Hata hivyo, mtoto aliyezaliwa alinusurika kwa kudra za Mungu licha ya kuangukia sakafuni wakati anazaliwa na kuserereka hadi chini ya meza ya mapokezi.

  Waziri Mwalimu alisema tukio hilo limemsikitisha na kwamba Serikali haitanyamaza hasa kutokana na ukiukwaji wa Sera ya mama na watoto inayoeleza ni lazima akina mama wajawazito na watoto wapewe huduma bora ili kulinda afya zao.
  "Nimesikitishwa sana na jambo hili, kama Wizara yangu yenye wajibu wa kulinda sera ya watoto tunalaani na tutawasiliana na wenzetu kuchunguza kwa kina," alisema Mwalimu.

  Alisema anamtuma Mkurugenzi anayehusika na masuala ya watoto kwenda kukutana na wenzake wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kufanya kazi kama timu kwa ajili ya kuangalia namna ya kumfanyia uchunguzi mtoto huyo.

  Wakati Waziri huyo akitoa tamko hilo, habari kutoka Wizara ya Afya na kuthibitishwa na mume wa Kuluthum, Ahmadah Yahya zinasema timu ya watu wanne kutoka Wizara hiyo na Hospitali ya Amana imekwenda nyumbani kwao eneo la Majohe kwa ajili ya mahojiano.

  Akiongea kwa njia ya simu, Yahya alikiri kupokea ugeni huo na kueleza walikwenda hapo kwa ajili ya kumuhoji mambo mbalimbali kuhusiana na tukio hilo.

  Alisema waliofika nyumbani kwake ni pamoja na daktari mmoja na muuguzi kutoka wizarani, Afisa malalamiko wa hospitali ya Amana na mwanasheria.

  "Ni kweli wamekuja watu kutoka wizarani hapa nyumbani kwangu, wamenihoji kuhusu tukio lile pamoja na kuchukua picha ya mwanangu," alisema.
  Alisema walichoahidi kwake ni kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu pamoja na kumfanyia uchunguzi mtoto huyo japokuwa hawakutoa tarehe maalum ya kumfanyia uchunguzi.

  Awali wabunge hao wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Philipa Mturano, walimtaka waziri Dk. Hussen Mwinyi, kuwachukulia hatua wauguzi waliosababisha uzembe huo pamoja na kuchunguza vyeti vya wauguzi wote nchini.
  Mturano alisema tukio lililompata mwanamke mwenzao limewasikitisha wabunge wote wanawake na kwa pamoja wameamua kuungana kulifuatilia jambo hilo hadi hapo haki itakapopatikana.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Unalaani tu halafu inakuwaje? Nilidhani jukumu la kulaani liwe la watu/vikundi vya kawaida. Serikali ni ya kuchukua hatua sio kuishia kulaani
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kama sasa serikali inalaani matokeo yaliyotokea sisi raia tufanyaje?
   
 4. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Hivi AMANA kuna pepo gani pale? Mbona kila siku mabalaa?
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kulaani ndo kufanya nini tena? Nafikiri ingekuwa busara kuona serikali inachukua hatua kuzuia kujirudia kwa tatizo hilo.
   
 6. E

  ELX JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 259
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 60
  Hivi kwanini amana kila mara?
  Inasikitisha sana ni hospital kubwa ila vitendo vyake vinatisha kila kukicha. Ukiambiwa na akina mama wanaoenda kujifungua pale inatisha na imekuwa kama desturi. Watu wanareport matatizo lakini hakuna mabadiliko, jamani watazania tumefika wapi?
  Mfano mwezi wa tatu wife alienda pale akiwa na uchungu wa kujifungua, kufika akaambiwa wewe bado urudi nyumbani, wakati hali haikuwa nzuri ya mtu kurudi, ikabidi wakomae palepale kusubiria, ikafika muda daktari akaja kuwaangalia wagonjwa akawaeleza manesi kuwa mbona anadalili zote za kujifungua? Ikabidi wampeleke "leba" alipofikishwa nesi akaondoka zake hana mpango na mgonjwa anamwambia bado sana.
  Kiukweli mwacheni mungu aitwe mungu-mke wangu aliweza kujifungua pasipo msaada wa nesi karibu, alipogeuza yule nesi tayari mtoto alisha toka kalala pembeni eti anasituka, ooh umeshajifungua, bali alitumia uungwana kidogo kumuomba samahani kwa kutokuwa karibu.
  Sasa je ndo ingekuwa kunamatatizo na anahitaji msaada wa haraka nini kingefuata?
  Jamani tuoneane huruma, sasa hapo maana ya hospital ni nini? Tutawalaumu watu kwanini hawaendi kujifungulia hospital?
  Hospita ya amana ibadilike hasa katika kitengo cha uzazi (mama na mtoto).
   
 7. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haya ndiyo matatizo ya watu kulazimisha fani ambazo sio zao. Unesi ni wito, mtu mwenye wito hufanya kazi kwa moyo wote.
   
 8. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  daktari anakuwa ni wa kutoka visiwani huyo
   
 9. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu kabla hatujalaumu fani tujiulize, je kuna vitanda vya kujifungulia vya kutosha? Nikiwa muhimbili nimeshuhudia mama akijifungulia sakafuni kwani vitando vyote labour ward vilikuwa vina wakina mama wengine. Hivi hapo nani Wa kulaumiwa???
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Only in Tanzania! Waziri analalaminika, Rais analalamika....pxmbxfu kabisa! Wale uamsho wanakosea sana kuita muungano dubwana. Dubwana ni CCM.
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yaani mpaka wabunge watishie kupeleka hoja bungeni ndio wizara zinaanza kutoa statements...hivi kwanini serikali yetu isiongozwe na wabunge?? maana ndio wanaonekana wachapa kazi kuliko mawaziri wenyewe
   
 12. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Serikali legelege, maamuzi legelege.
   
Loading...