Serikali yakerwa kufukuzwa wanafunzi Ndanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yakerwa kufukuzwa wanafunzi Ndanda

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by thatha, Jan 21, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Serikali yakerwa kufukuzwa wanafunzi Ndanda

  • Yaruhusu wafanye mtihani

  na Abdallah Khamis  Mbali na hatua hiyo, wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita waliofukuzwa wataruhusiwa kufanya mitihani yao ya mwisho bila wasiwasi wowote.
  Uamuzi huo umefikiwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, mara baada ya kupokea maandamano ya amani ya vijana wa Kiislamu yaliyokuwa na lengo la kupinga kile walichokiita dhuluma, ubaguzi, unyanyasaji na uonevu wanaofanyiwa katika ngazi mbalimbali za kielimu nchini.
  Katika malalamiko hayo, wanafunzi hao wa Kiislamu walilalamikia hatua ya uongozi wa sekondari ya Ndanda kuwatimua wenzao 20, na kumtaka Waziri Kawambwa awe amewarudisha shuleni ndani ya siku tano.
  Hata hivyo, pamoja na kuwakubalia maombi yao mengine, Kawambwa aliwataka waache shinikizo hilo, badala yake wavute subira kwa kuwa serikali imekubali kuwasaidia.
  Akizungumza huku akiwa amezungukwa na umati mkubwa wa vijana wa Kiislam kutoka shule za sekondari na vyuo vilivyoko jijini Dar es Salaam, Waziri Kawambwa alisema adhabu iliyotolewa kwa vijana hao si sawa na kwamba wizara yake italishughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha wote waliohusika na kuleta mkanganyiko wa kiimani katika shule hiyo.
  “Ni kweli leo niko hapa na ninyi katika mkusanyiko huu kujadili suala ambalo tayari nilishaongea na viongozi wenu juzi, na tukakubaliana mambo ya kufanya na kwa kuwa ninyi mlitaka kuonana na mimi ninachoweza kuwaahidi ni kwamba tunalishughulikia suala hili, na kilichofanyika Ndanda si sawa kwani kuna adhabu nyingine zinazoweza kuwa badala ya hii iliyotolewa kwa hao vijana,” alisema Dk. Kawambwa.
  Dk. Kawambwa aliyeongozana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, aliwataka vijana hao kuwa na uvumilivu kwa serikali yao kwa ajili ya kuenzi mwenendo wa Mtume Muhamad aliyewavumilia wale aliotofautiana nao.
  Naye Kamanda Kova, alisema Uislmau ni ishara ya amani na kuwataka vijana waliokusanyika katika viwanja hivyo wahakikishe amani inatawala mpaka mwisho wa mkutano huo.
  Mapema Rais wa Taasisi za Kiislamu Tanzania (Tamsiya) Sheikh Jaffar Mneke akisoma risala yake kwa Waziri Kawambwa, alisema vijana wa Kiislamu nchini wamechoka kudhulumiwa katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoj na kufanywa kuwa watu wa daraja la pili katika nchi yao.
  Alisema tukio la Ndanda linadhihirisha jinsi vijana wa Kiislamu wanavyokumbana na wakati mgumu wa kutekeleza ibada kwa misingi ya imani yao kwa visingizio vya ratiba ya vipindi ilhali serikali ilishatoa miongozo kwa shule za serikali kwa ajili ya watu wa imani tofauti kutekeleza imani zao.
  “Mheshimiwa waziri ndugu zetu wa Ndanda wanakashfiwa waziwazi na mkuu wa shule na baadhi ya maneno ni kama vile alivyowaeleza kuwa wawaombe viongozi wa kanisa eneo la kufanyia ibada kwa kuwa shule hiyo ilikuwa ya kanisa kabla ya kutaifishwa”
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Malaria Sugu ameileta hii stori,jamaa wameifunga,i mean m0ds,iachen jama
   
 3. wajaleo

  wajaleo Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  thats it
   
 4. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 5. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 6. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 7. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 8. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hongera mh. Shukuru kawambwa...

  tunajua wale wa
  mfumo wamechukia lakini "no way out"
   
Loading...