Serikali yajitosa mgodi wa mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yajitosa mgodi wa mkapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Oxlade-Chamberlain, Jun 6, 2009.

 1. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Serikali yajitosa mgodi wa Mkapa
  Na Mwandishi wetu  6th June 2009  [​IMG]
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

  [​IMG]
  Rais mstaafu, Benjamin Mkapa.

  [​IMG]
  Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]  Kuna dalili kubwa za serikali kuutwaa mgodi wa Mawe Kiwira kutoka mikononi mwa wawekezaji ambao Kampuni ya Tanpower Resources Ltd ambayo inamilikiwa na familia ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema taarifa ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mgodi huo ataitoa bungeni na kwamba, serikali imeamua kukwamua mradi huo.
  Taarifa ambazo zilipatikana kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, zilidai kuwa miongoni mwa mapendekezo iliyopeleka serikalini ni kuchukua mradi huo kwa sababu, mwekezaji ameshindwa.
  Pia, kamati hiyo ilitaka kujua sababu zilizosababisha fedha zilizotolewa na serikali kwa mwekezaji hazikufanya kazi iliyokusudiwa.
  Tanpower Resources Ltd, inayomilikiwa kwa pamoja na familia ya Mkapa na Yona, ilimilikishwa mgodi huo na ulikuwa umepangwa kukamilika mwaka huu, lakini umekwama na hadi sasa wafanyakazi wanadai mamilioni ya fedha kama malimbikizo ya mishahara. Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana, Ngeleja alisema serikali imeamua kukwamua uendelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza ya kuzalisha umeme wa megawati 200.
  “Kama mambo mengine yasingetokea mwaka huu tungeanza kuzalisha umeme wa megawati 200...pale kuna madai ya wafanyakazi yanakaribia Sh. bilioni moja,” alisema Ngeleja na kuongeza: “Serikali imeamua kukwamua uendelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo wa umeme wa Kiwira wa Mw 200 uliokuwa umepangwa kukamilika mwaka 2009 ili uweze kukamilishwa mwaka 2011.”
  Hata hivyo, Ngeleja hakutaka kubainisha hatua zitakazochukuliwa kwa sababu, amekubaliana na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kuwasilisha taarifa bungeni.
  “Nikitamka hapa kitakachonitokea ni kikubwa...subiri nitatoa taarifa bungeni,” alisema na kuongeza kuwa, baada ya miezi 18 tangu kuanza kwa mradi wa Kiwira zitakuwa zinazalishwa megawati 200.
  Serikali inamiliki asilimia 15 ya hisa katika mgodi huo wenye thamani ya Sh bilioni nne, lakini uliouzwa kwa akina Mkapa kwa Sh. milioni 700 lakini wakakabidhiwa kwa kulipa Sh milioni 70 tu.
  Taarifa za ndani ambazo Nipashe imezipata, zinasema kwamba mgodi huo kwa sasa hauzalishi hata megawati moja isipokuwa unazalisha makaa ya mawe kati ya tani 50 na 100 kwa siku.
  Suala la mgodi wa Kiwira limekuwa tete na limezua mjadala mkubwa nje na ndani ya Bunge, huku baadhi ya wabunge wakituhumu uuzaji huo kuwa ni uporaji wa wazi wa rasilimali za umma.
  Kuhusu maendeleo ya sekta ya nishati, Ngeleja alisema miradi mbalimbali inaendelea na ikikamilika wanatarajia itaimarisha upatikanaji wa umeme na kupanua wigo wa wateja kutoka asilimia 14 ya Watanzania wanaonufaika hivi sasa.
  Alitaja wafadhiliwa miradi hiyo kuwa ni Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Mellenium Challenge Cooperation (MCC), Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (Jica) na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (Sida). Ngeleja alisema licha ya miradi ya Kinyerezi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, mradi wa kuzalisha nishati hiyo kwa upepo mkoani Singida mwakani utakuwa umeanza uzalishaji kwa k uanzia na megawati 50.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Duu Mkapa ameshapiga pesa kibao alizokopa ajili kuendeleza hicho kiwanda balaaa jamani hawa jamaa wamepiga bao sasa wanajifanya wako kimya....wangeiburuza mahakamani wote....
   
 3. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukitembelea Mgodi wa KIWIRA na ukiangalia bei waliyonunulia huo mgodi unaweza kupata uchizi. Hawa watu wanatakiwa wanyang'anywe faster huo Mgodi na uzalishaji uendelee mara moja. Hawa jamaa ni zaidi ya MAFISADI
   
Loading...