Serikali yajipanga kuajiri walimu 4,900

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,552
2,000
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeomba kibali cha kuajiri walimu mbadala 4,900 wa masomo ya sayansi katika shule mpya za sekondari zinazojengwa nchini hivi sasa, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wanafunzi isiyoendana na uwiano wa walimu uliopo.

Ombi hilo limewasilishwa kwenye Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, baada ya kuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, kukosa nafasi kutokana na uhaba wa madarasa. Akizungumza na gazeti hili jana, Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Tixon Nzunda alisema wanafunzi waliofaulu na kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni 133,747, hivyo mikoa iliyokuwa na uhaba wa madarasa, ilipewa maelekezo ya kujenga vyumba hivyo hadi ifikapo Februari mwaka huu.

“Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani Jafo wakati akitangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwishoni mwa mwaka jana, alitoa muda wa miezi miwili kwa mikoa iliyokuwa na uhaba wa madarasa, kuhakikisha wanakamilisha ifikapo Februari mwaka huu, ili wanafunzi waliokosa nafasi wachaguliwe kwenye awamu ya pili hapo Machi, sasa mwitikio ni mkubwa na baadhi ya mikoa imejenga shule mpya za sekondari,” alisema Nzunda.

Awali Jafo alisema mikoa iliyokuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa ni Arusha ambayo jumla ya wanafunzi 18,719 walifaulu na kukosa nafasi, Dodoma (5,991), Iringa (2,774), Kagera (14,046), Kigoma (12,178), Lindi (1,294), Mara (16,356). Mingine ni Njombe (3,172), Mbeya (6,395), Simiyu (12,684), Rukwa (4,930), Tabora (11,209), Tanga (5,400), Manyara (5,392), Shinyanga (6,271), Katavi (1,249) na Pwani (4,731). Akizungumzia mwitikio wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, Nzunda alisema baada ya Jafo kuagiza mikoa na halmashauri zote nchini zilizokuwa na uhaba wa madarasa kuhakikisha wanajenga, agizo hilo limetekelezwa kwa asilimia kubwa ambapo mikoa mingine imejenga shule mpya ukiwemo Mkoa wa Mbeya.

Nzunda alisema changamoto inayoonekana sasa ni kuwepo kwa shule nyingi mpya zilizojengwa, ambazo hazina rasilimali watu yaani walimu na hivyo wameomba kibali Utumishi kwa ajili ya kuajiri walimu wa sekondari, hususani wa masomo ya sayansi wapatao 4,900. “Nimezunguka mikoa mbalimbali kuangalia ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza waliokosa nafasi na mwitikio ni nzuri, wananchi wanasaidiana na wadau wa maendeleo na serikali kujenga na shule mpya nyingi ziko hatua ya mwisho, hivyo tumeona tuombe kibali cha ajira mbadala za walimu na tunaamini tutapewa na kuajiri,” alisema Naibu Katibu Mkuu Tamisemi.

Alisema wameamua kuwapa muda wa hadi Februari 28, mwaka huu mikoa yote yenye upungufu wa madarasa kukamilisha; na baada ya hapo watafanya thathmini yake sambamba na kufanya uchaguzi awamu ya pili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza, unaotarajia kufanywa mapema Machi mwaka huu. “Ipo mikoa imeshatekeleza ujenzi wa madarasa na mingine inaendelea kujenga na baadhi wameamua kujenga shule mpya kabisa.

Mfano Mbeya kule Chunya wao wamejenga shule mpya na sasa wanapiga ripu na rangi, tuna uhakika kwamba mwisho wa Februari mwaka huu, asilimia 90 ya wanafunzi waliokosa nafasi watachaguliwa kwenye awamu ya pili,” alifafanua. Alisema Mkoa wa Arusha ambao jumla ya wanafunzi 18,719 walifaulu na kukosa nafasi kutokana na uhaba wa madarasa, watendaji wamechukua hatua za ujenzi na sasa wanaendelea kukamilisha ili idadi hiyo ya wanafunzi wapate nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Katika hatua nyingine, Nzunda alisema wanatarajia kutangaza ajira 7,000 za walimu wa elimu ya msingi na sekondari kabla ya Juni mwaka huu ili kukabiliana na uhaba wa rasilimali watu hao katika shule mbalimbali nchini. Mwishoni mwa mwaka jana, Waziri Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu ni 599,356, sawa na asilimia 81.76 ya wanafunzi 733,103 waliofaulu.

Chanzo: Habari Leo
 
100miles

Member
Oct 30, 2018
50
125
Bila shaka hizi zinatakuwa ni tifauti

Bila shaka hiz ajira 4900 zitakuwa ni tofauti na zile ajira za mwanzo walizozisemea ambazo ni 6000, za waalimu wa sayansi,anyway, naomba wafanye haraka iwezekanavyo ili ndgu zetu wakapate elimu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom