Serikali yaikana Malawi ramani ya Ziwa Nyasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaikana Malawi ramani ya Ziwa Nyasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 5, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Fidelis Butahe na Aidan Mhando

  SAKATA la mgogoro wa Ziwa Nyasa limezidi kuchukua sura mpya baada ya Serikali ya Tanzania kupingana na kauli ya Rais wa Malawi, Joyce Banda aliyetangaza nchi hiyo kujitoa katika mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo baada ya kubaini kuwa Tanzania imezindua ramani mpya inayogusa mipaka ya ziwa hilo.


  Kauli hiyo ya Banda aliyoitoa juzi ilionekana wazi kufifisha matumaini yaliyokuwa yameanza kupatikana kupitia mazungumzo hayo.

  Jana Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilisema mabadiliko ya ramani ya taifa hayahusiani na mgogoro wa Malawi na Tanzania katika Ziwa Nyasa.

  Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa wizara hiyo, Dk Selassie Mayunga aliliambia Mwananchi kuwa mabadiliko ya ramani yanatokana na kuongezwa kwa mikoa mipya pamoja na wilaya, lakini hayahusiani na mgogoro uliopo.


  “Ni kweli kuna mabadiliko ya ramani ya taifa lakini mabadiliko haya yanatokana na kuongezeka kwa mikoa na wilaya mpya,” alisema Dk Mayunga na kuongeza:

  “Mipaka ya nchi katika mabadiliko ya ramani hii imebaki kama ilivyokuwa enzi za ukoloni na hatuwezi kufanya mabadiliko ya mipaka hiyo.”
  Dk Mayunga alibainisha kwamba siyo vyema mabadiliko hayo yakahusishwa na mgogoro wa Tanzania na Malawi kwa kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ramani ya Taifa na ramani ya mipaka hiyo.

  “Tumeamua kufanya mabadiliko hayo hasa kwa kutambua kwamba kuna mikoa mipya minne na wilaya 19 jambo ambalo lilikuwa na ulazima wa kutoa ramani mpya ya kuonyesha wilaya hizo na mikoa hiyo ili wananchi wafahamu mipaka ya maeneo yao,” alisema.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule alipoulizwa kuhusu suala hilo alitaka apewe muda ili azungumze na mabalozi wanaoziwakilisha nchi hizo kila upande, ili kutoa jibu sahihi.

  Uamuzi wa Malawi kujitoa katika mazungumzo hayo, umekwenda sambamba na kufutwa kwa ziara ya Rais Banda nchini, hatua ambayo inazidisha mgogoro baina ya nchi hizi mbili.

  Rais Banda alisema tayari ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi yake, kujitoa katika mazungumzo hayo kutokana na kile alichodai kuwa ni vitendo vya Tanzania kutoashiria utafutaji wa suluhu kwa njia ya amani.


  Rais Banda alitoa agizo hilo alipokuwa akilihutubia taifa hilo baada ya kurejea nchini kwake akitokea Umoja wa Mataifa (UN) alikokuwa kwa ziara ya kikazi.


  "Wakati naondoka kwenda UN nilidhani suala la mpaka wa Malawi na Tanzania lilikuwa likihitaji mazungumzo, lakini nikiwa huko nikasikia kwamba Tanzania imezindua ramani mpya inayogusa ziwa hilo," alisema Banda na kuendelea:

  "Baada ya hatua hiyo wavuvi wa Malawi wameanza kufukuzwa ufukweni na boti zetu zinaondolewa Tanzania. Ni suala zito sasa ambalo tunatakiwa kuchukua hatua nyingine," alisema.

  Alisema mbali na kuzinduliwa kwa ramani, pia alishangazwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa na kuilaumu nchi yake kwamba inawazuia Watanzania wasitumie maji ya Ziwa Nyasa.

  Banda alisema akiwa UN alijadiliana na Katibu Mkuu Ban Ki-moon kuhusu suala hilo kwa lengo la kupata mawazo kabla ya kulifikisha suala hilo Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ).

  Kuvunjika kwa mazungumzo hayo kumekuja baada ya kuwapo kwa vikao kadhaa vilivyofanyika nchini Malawi na Tanzania, ambavyo hata hivyo, havikuweza kupata mwafaka.


  Alipotakiwa kuzungumzia hatua hiyo ya Malawi alisema," Ndiyo kwanza nasikia kwenu. Sijapata mawasiliano na waziri ila ninachojua, ndani ya mwezi huu (Oktoba) mazungumzo hayo yataendelea."


  Serikali yaikana Malawi ramani ya Ziwa Nyasa
   
 2. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,521
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  hiyo kauli ni kama tunaambiana sisi wenyewe,nilitegemea kauli ya rais kama majibu kwa mama Banda.. Kama jk hawezi kutoa kauli za kutetea mipaka awaachie aliowaita wapinzani.!
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hii kauli hapa chini ni ya nani? Nyembe ama jk?
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Mkuu King'asti ni Rais Banda wa Malawi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Dr, hii habari inajicontradict ndo maana nikauliza hivyo. Sasa kama rais wa malawi hajui kama wao wameikana tz kwenye issue ya mpaka na wameipeleka UN, na anaendelea kusema anategemea mazungumzo kuendelea this month. Ina maana gani? Hebu soma tena habari origina uone hii
   
 6. epson

  epson JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45

  Attached Files:

Loading...