Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza uhamasishaji wa kuwavutia Wawekezaji watakaosaidia kuwapeleka watalii katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa baada ya Serikali hiyo kuweka miundombinu wezeshi ya Utalii katika maeneo hayo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya ya Burigi, Biharamulo, Kimisi,Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi ya Taifa.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku moja uliofanyika jijini Mwanza baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali nchini, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Sekta binafsi ni injini ya Utalii nchini.