Serikali yabaini bandari bubu ya dawa za kulevya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Serikali imewaagiza watendaji wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanafanya operesheni maalum ya vyombo vya ulinzi na usalama katika eneo la bandari bubu ya Kigombe iliyopo pembeni mwa bahari ya hindi,baada ya kubaini kuwepo kuwa eneo hilo ndio lango kuu la uingizaji dawa za kulevya,usafirishaji wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya kenya na uvuvi haramu wa mabomu.

Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga,watendaji wa serikali pamoja na wananchi wa eneo la Kigombe,Naibu Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Mheshimiwa William Ole Nasha amesema ni lazima operesheni zifanywe kila wakati kwa sababu eneo la kigombe limebainika kuwa ni kunafanyika uhalifu wa kimataifa ikiwemo kusafirisha binadamu kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Awali Mbunge wa Jimbo la Muheza Mheshimiwa Balozi Adad Rajab amesema mbali na uhalifu wa kimataifa kufanyika katika eneo la Bandari ya Kigombe,pia vijana wengi wamekuwa wakitumia vyombo vya majini kusafiri na kwenda nje ya nchi na wanapofika huko wanakabiliwa na tatizo la ubebaji na matumizi na utumiaji wa dawa za kulevya.

Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi katika eneo hilo,wameiomba wizara husika kuhakikisha kuwa wanatoa motisha kwa ajili ya kuwawezesha wajumbe kutaja majina ya wavuvi haramu wa mabomu ambao baadhi wanatokea nchi jirani ya Kenya kwa sababu kipato walichonacho na kazi ya kuwataja wahalifu inahatarisha maisha yao.

Chanzo: ITV
 
Nafikiri Tanga ni mkoa unaoongoza kwa bandari bubu nchini, kuna zaidi ya bandar bubu 40, kule vitu vya haramu vingi hupitishwa. Na sina shaka jeshi la ulinzi mkoa linazifahamu ila zinashindwa kuzidhibiti na kuiachia kazi TPA na SUMATRA wafanye patrol ambazo hufanyika mara chache sana. Nilishangazwa sana na hali hiyo nilipokua Tanga 2014.

Serikali iongeze nguvu ya jeshi zile bandari bubu zote zisambaratishwe ama zitaifishwe TPA kama zitakuwepo zinazokidhi viwango.

Nafurahi kuona serikali sasa inamuelekeo wakudhibiti, wasiishie madawa ya kulevya tu, kule mafuta, sukari na vipodozi hatarishi hupitishwa na kuhatarisha afya za Watanzania.
 
Haya maigizo yanaichelewesha Tanzania

Badala ya kufunga hiyo bandari bubu

kwa nini wasideal kwanza na WAASISI wake

Hao ndio Tatizo!


Maana swali la msingi ni kwamba

Je bandari hizo zina uhusiano na waliotajwa?

Kama hazina,

Bandari mpya feki zitaanzishwa si muda mrefu

Jamaa watabadili tu style

But biashara kama kawa!

Kuna njia za kusolve haya

Sio Hizi!
 
Tanga yenyewe imeshakufa sasa tena wanaenda kuifukia kabisa duh haya tokeni wajameni njoeni darisalama tubanane.
Sitetei bandari bubu ila zingeboreshwa vijana wapate ajira.sasa unapoziua kabisa na mbadala hakuna unategemea nini?haya na Uvuvi nao masharti.kilimo nafkiri pale ni mihogo au kuna mazao mengine?
 
Bandari bubu
Vyeti kiziwi
Watumishi hewa
Mateja feki
ARV batili
Kocha Bomu
Tanzania ya viwonder...kaaaazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom