Serikali yaahidi walioua mtalii kukamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaahidi walioua mtalii kukamatwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 24, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 23 June 2012 10:01 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [​IMG]

  Mussa Juma, Dodoma


  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, wamemhakikishia Balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek, kuwa majangili wote waliohusika na mauaji ya mtalii Eric Brekelmans(53) wanakamatwa.

  Hatua hiyo inafuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete, kuwaagiza mawaziri hao kufuatilia mauaji hayo, hali iliyosababisha kukatisha kuhudhuria vikao juzi kwenda Arusha kukutana na Balozi Koekkoek na mjane wa Brekelmans, Annelnes.

  Kifo hicho kilitokea katika Kambi ya Moivaro,Kijiji cha Robanda, kwa kupigwa risasi na majangili.
  Mawaziri hao, waliondoka kwa ndege ya Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) juzi mchana mjini Dodoma kwenda Serengeti kufuatilia tukio hilo.

  Pia, majangili hao walimuua Meneja msaidizi wa kambi hiyo, Renatus Bernard na watalii wengine 40 waliporwa mali zenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni.

  Wakizungumza juzi usiku mjini Arusha na balozi huyo na mjane nyumbani kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Leopard, Zuher Fazal,mawaziri hao walitoa pole kwa tukio hilo ambalo walisema siyo la kawaida na ndiyo maana walitumwa na Rais Kikwetekwenda eneo la tukio.

  Balozi Kagasheki alisema,tukio hilo limeisononesha Serikali na Watanzania kwa ujumla, kwani dunia nzima inatambua amani na utulivu uliopo nchini.

  Dk Nchimbi alisemaSerikali itahakikisha wote waliohusika na mauaji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

  Naye mjane Brekelmans, Annelnes aliishukuru Serikali ya Tanzania, kwa ukaribu ilioonyesha na kwamba, mumewe aliuawa kwa kupigwa risasi kifuasi wakati akipambana na majangili hayo, huku yeye akijeruhiwa kwa panga.

  Hata hivyo, Annelnes alisema usalama katika kambi hiyosiyo mzuri, kwani ina eneo kubwa na hakuna usalama wa kutosha, jambo ambalo alishauri lirekebishwe.

  Kwa upande wake,Balozi Dk Koekkoek alieleza kusikitishwa na tukio hilo, huku akimshukuru Rais Kikwete, mawaziri hao na watu wengine ambao wamekuwa wakishirikiana naye tangu tukio hilo kutokea[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...