mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,514
- 6,070
Kwa kuwa suala la amani ni jukumu la kila mtanzania kabla ya wizara yenye mamlaka husika moja kwa moja. Ni kwa nini wenye mamlaka husika wasingewaweka wazi watu hawa wabaya ili sisi raia tuwatambue kuliko kutupa jiwe gizani?
================
Watanzania wameombwa kuendelea kudumisha muungano, kuitunza amani pamoja na kuwaunga mkono viongozi mbalimbali wanaowaongoza ili wazidi kuleta maendeleo nchini.
Hayo ameyaeleza Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah leo Aprili 25,2025 kwenye maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa mkoani Mtwara katika Manispaa ya Mtwara Mikindani huku kitaifa yakitarajiwa kufanyika Jijini Dodoma.
Aidha amewahakikishia watanzania hao kuwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar itaendelea kuilinda amani ya nchi na kudumisha muungano.
"Serikali haitasita kuchukua hatua kwa mtu, kikundi cha watu au taasisi ambayo itabainika kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani ya muungano."Amesema Abdulla