Serikali ya Tanzania yajipanga kuteka soko la watalii China

mla dindili

Senior Member
Nov 8, 2018
110
79

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii, suala la kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.

Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS

Amesema lengo mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya
China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.

Mkutano huo umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho,Prof.Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.

Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao

Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili kujengeana uwezo baina ya Serikali ya Tanzania na China
 
China hakuna watalii watu wanosifika kwenye maswla ya utalii ni wazungu wao ndo huweza kuhifadhi hela miaka 5-10 ili waende wakatalii sehemu fulani lakini sio wachina
 
Wachina walio wengi ni maskini. Baada ya ku promote utalii kwenye nchi za magharibi wao wanahangaika na hiyo mijitu
 
Kila siku, kila saa, kila dakika lazima apite mchina hapa ila sasa wengi wao ni wale madubwasha ya kuchezea BONANZA,,, unaweka 100,000/= unapuna 20,000/= mtaji ni 200/= tu huyo madubwasha yupo mpaka vilabuni, mpaka kwenye maduka na kwenye mabaa ..
 
Back
Top Bottom