Serikali ya Tanzania ukihoji kwa nini, utapotezwa

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
949
Serikali ya Tanzania ukihoji kwa nini, utapotezwa. Ukweli unageuzwa kuwa uchochezi, taasisi za serikali zipo makini kwenye kulinda maslahi ya viongozi na maslahi ya yao binafsi mfano ulio hai ukitukana Mtandaoni sasa hivi TCRA hadi kufikia kesho wamekupeleka POLICE.
Viongozi wetu furaha yao kuongoza watu wajinga ukijaribu kuhoji kwa nini, unapotezwa na ukijaribu kufuwafuatilia unapotezwa kama Sokoine au Chache wangwe.
Serikali inatumia pesa nyingi na nguvu kubwa kulinda wanyama pori, haijali usalama wa mtanzania .Serikali inatumia mbinu zile zile za kipindi cha serikali ya Hayati Nyerere.

Viongozi wetu wapo juu ya sheria, hamna utawala wa sheria kiongozi anavamia chombo cha habari na hakuna kilichofanyika juu yake, yupo na atazidi kuwepo madarakani. Haki inapindishwa Mhe. Nape katumbuliwa kwa kuunda tume iyoleta majibu sahihi mharifu kaachiwa madaraka tu.

Katika awamu hii utekaji umekuwa kawaida sana na jeshi la polisi hawatoi majibu la kueleweka. usalama wa mtanzania upo lehani. hatuwezi kwenda UCHUMI WA VIWANDA wakati usalama wetu ni duni, hata wawekezaji wanapata hofu. Maendeleo hayawezi kuja sehemu isiyokuwa na amani, Tanzania kuna UTULIVU NA UWOGA ila hakuna AMANI.

Kwa kipindi hiki TUNAVUMILIA KUWA WATANZANIA ILA HATUJIVUNII KUWA WATANZANIA.

Takwimu za B.O.T za uongo zinasema uchumi wetu unakua, haziendani na uhalisia. IMF wametoa ripoti na takwimu sahihi za uchumi wetu na sera mbovu zinazotumika kuinua uchumi wetu. Deni la taifa linazidi kukua, hii nchi hatuja fika kujipangia bajeti bila kupewa pesa na waisani na ilibidi twende pole pole na mikakati ili tufike pahala pa-kujipangia bajeti yetu.

Uchumi wetu mpaka hapa tulipo umechangiwa na sera mbovu za chama tawala na uongozi mbovu wa chama hiko, Tanzania ni nchi yenye serikali ya ufalme wa kichama.
 
Back
Top Bottom