kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,633
- 7,022
Tuliomba nafasi ya kusoma diploma ya kozi za Afya kupitia NACTE,mkatupangia vyuo binafsi,wachache wakapata vyuo vya serikali.Hao waliopata serikali mmeamua kuwadhamini ili wakimaliza wafanye kazi serikalini.Sasa napenda kujua hili,ni kwa nini sisi tuliopangiwa vyuo binafsi tusipewe angalau mkopo katika pesa hizo mnazopeleka kwa wanafunzi walio kwenye vyuo vya serikali pekee?
Upo ushahidi kuwa hao waliopata vyuo vya serikali wapo wenye uwezo mkubwa wa kulipia private japo mmamua kuwapa ruzuku wao peke yao.Pili ni ukweli usiofichika kuwa wengi mliowachagua huko wengi wetu tumewazidi uwezo na ufaulu wetu ni mkubwa ijapo tumesoma shule za kata,ni kwa nini basi serikali ikatupangia tuje vyuo binafsi wakati nasi tulikuwa na haki nya kusoma vyuo vya serikali tupate ruzuku?
Natoa wito kwamba mfumo huu wa udahili uliopo ufutwe ili tupate nafasi ya kuchagua wenyewe vyuo tunavyotaka na tupate ushindani sawa kwenye vyuo vya serikali na ikibidi uwepo mtihani mwingine ili haki itendeke.
Nina masikitiko sana kwa hili kwa kuwa wako wengi wanaoumia huku private ambao wanazo hata sifa za kusoma university na walikosa tu nafasi kwa vile zilikuwa kidogo ingawa wako eligible.Naomba mkifanya maamuzi muwe mnafanya ya haki vinginevyo Mungu anawaona.
Mimi ni sauti ya mnyonge.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni