Serikali ya Mseto yanukia

Kutounga mkono kwako hakubadilishi kitu.

matamshi hayo wameyasema makada wa ccm ambao ni mabalozi wastaafu na kikosi kazi cha samia ambacho kimejaa makada nguli wa ccm, na habari imeripotiwa na gazeti la mwananchi ambalo mmoja wa wanahisa wake ni ccm.

Hakuna chama cha upinzani hapo, mnakanyagana ninyi wenyewe
 
Chaguzi nyingi za Afrika ni kufa na kupona sababu Mshindi anabeba Kila kitu na ulishindwa hata kwa kura 10 basi unakosa Kila kitu.

Serikali ya mseto Ina maana hata mtu akiangushwa basi ana consolation ya ku exercise malengo yake ya kiuongozi kupitia serikali ya mseto.

Hata Kenya solution ndio hiyo that's why hausikii maandamano tena ya walimu sijui wafanyakazi n.k.

Ni wazo jema sema kwa Zanzibar imekuwa ceremonial zaidi kuliko kiutendaji ndio maana inaonekana kama ipo kiulaghai tu but kama ikiwekewa structure nzuri itapunguza political tensions Bara na visiwani hasa nyakati za uchaguzi
 
Uzungumzia nchi ipi hiyo we jamaa?
 
Sukuma gang bado mnaota ndoto za kuua na kutesa wapinzani kama alivyowazoesha.

Mama hataki hayo na wala hataki ushauri wenu. Kaeni pembeni, zama zenu zimepita.

Kama inawauma nendeni mkazikwe naye Chato.
Kwann mseto, sukuma ccm wote nje ya utawala kisha futa kabisa jilo lichama
 
Acha kejeli wapinzani walikua na wabunge 120 between 2015-2020 tena hapo ni baada ya majimbo kma Kigoma kusini, Nyamagana, Kasulu mjini, Segerea,Kahama n.k rafu kuchezeka. So upinzani Una uwezo wa kushinda majimbo zaidi ya 150 kama uchaguzi ukiwa huru na haki.

Hivi kama 2010 licha ya tume mbovu upinzani ulipata 38% ya kura za Urais... 2015 upinzani ukapata 43% kura za Urais na kura zaidi ya 45% za ubunge nini kinakuaminisha wapinzani hawawezi shinda majimbo 100 kama wanaweza pata kura average 40% za wananchi wote???
 
Sasa Kama upinzani hauwezi kushinda majimbo mengi , wale askari Na majeshi waliokuwa walipita watu Na kupeleka masanduku ya kura ni ya kazi gani ?
Baada ya kupatikana KATIBA mpya 2026, itazaliwa TUME huru ya Uchaguzi.

Matokeo ya Ubunge na Urais yatahojiwa mahakamani.

Chama Dola ukikitenganisha na MATUMIZI ya Dola hakiwezi simama.

Wananchi wataamua. Mungu ni Mwema sana.

Ni TANZANIA pekee tumepata neema ya kuandika KATIBA mpya bila kutumia matone ya DAMU ya Watanzania.
 
Nasubiria kikosi KAZI cha katiba mpya KWA HAMU Sana!
 
Labda kitatawala Burundi
Punguza hasira comrade rudisha kadi na usubirie chama KIPYA!mauaji ya Ngoro ngoro yanatosha KABISA kuzamisha jahazi!!Tumekiua chama WENYEWE KWA kuendelea uchawa na dhulma kwq wananchi!!!wenye hekima wamewekwa kapuni machawa ndio wameula na yanakiua CHAMA !!!!!
Fanya maandalizi KABISA!

Chama kimejiua chenyewe!!
 
Chama cha watu WA Burundi kinanihusu vipi mimi?
 
Nasubiria kikosi KAZI cha katiba mpya KWA HAMU Sana!
Maoni yalishatolewa na wananchi.

Ikirudishwa mezani Rasimu ya Warioba, tutahitaji Maboresho kadhaa kwakuwa muda umepita mrefu.

Hawatakusanya upya maoni. Ni wananchi waisome na kuielewa, mapungufu yarekebishwe na kuongezwa MAZURI mengine mf Idadi ya Serikali na MUUNGANO nk.

Unaweza ona kuwa AJIRA ya miaka 9 walioahidiwa kina KABWELA imeyeyuka rasmi.
 
Serikali mseto kwa kitu gani kwanza au kwa serikali ipi..?, Mama mnamuondoa kweny3me sekeseke la maovu wakati wa awamu ya tano leo mnamtaka ajenge umoja HOW?.
 
Imenikia kwenye magazeti labda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…