Serikali ya Mbeya: Pongezi....

Chipolopolo

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,425
725
Walianza kwa kupandisha ushuru hivi karibuni. Wananchi na wafanyabiashara wa wa eneo la Soko la Soweto Jijini Mbeya wakagoma kulipa ongezeko hilo. Ulikuwa mgomo ulioathiri shughuli zote za uuzaji na ununuaji eneo hilo. Maduka na vizimba vya biashara vilifungwa.Mabomu kama kawaida yalihusika katika kuwatawanya walioitwa wagomaji.Sababu ya mgomo huo ilikuwa na mashiko.

Hoja yao "Kwanini ushuru upandishwe wakati huduma haziboreshwi?" Eneo hilo la soko upande wa Kusini likuwa na madimbwi yatoayo harufu, maji kutuama mara mvua zinyeshapo.

Eneo hilo nimaarufu kwa kuuza samaki wabichi na wakavu, pia bucha za nyama.Haikubaliki kwa afya! Pamoja na wananchi kupigwa mabomu, serikali wamechukua hatua. Wameanza kutengeneza barabara nzuri eneo hilo na kuchimba mifereji ya maji.Tabia hii ya serikali inaweza kujenga picha ya kwamba bila migomo au maandamano haiwezi kutekeleza wajibu wake?Katika yote bado natoa pongezi kwa serikali ya jiji la Mbeya kuchukua hatua....
 
Back
Top Bottom