Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inadaiwa Bil. 106 na Tanesco

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
19,383
38,300
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inadaiwa bil 106 na shirika la umeme nchini Tanganyika Tanesco. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mhandisi F. Mramba. Endelea kusoma mwenyewe.

Tanesco yadai bn 250/- kila kona
BY ROMANA MALLYA
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), linaidai serikali ya
Tanzania, wateja binafsi na Serikali ya Zanzibar jumla
ya Sh. bilioni 250.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba,
wakati Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji
(EWURA), ilipowasilisha kwa wadau mapendekezo ya
kurekebisha bei ya umeme kwa asilimia 1.1,
yaliyoombwa na shirika hilo.
Katika ukusanyaji wa maoni, wadau walitaka kufahamu
deni hilo litalipwa lini.
Ndipo Mramba aliposema kuwa wanaodaiwa, ikiwemo
serikali ya Tanzania na ya Zanzibar wameahidi
kupunguza ifikapo Januari mwakani .
Mramba alisema katika deni hilo, serikali ya Tanzania
inadaiwa Sh. Bilioni 33 na ile ya Zanzibar Sh. Bilioni
106.
Zaidi ya Sh. Bilioni 110 ni madeni ya wateja binafsi,
alisema Mramba na kueleza zaidi kuwa kuwa lengo la
Tanesco ni kupunguza madeni hayo kwa asilimia 50
ifikapo mwakani.
Katika mkutano huo wadau walionyesha hofu kwamba
kama Tanesco haitajipanga kwenye ukusanyaji
mapato, mapendekezo hayo ya kupunguza bei
hayatadumu kwa muda mrefu.
Tanesco imependekeza kupunguza bei ya umeme
kuanzia Aprili 1 kwa asilimia 1.1 na mpaka kufikia
Januari mwakani nafuu hiyo iwe imefika asilimia 7.9.
Aidha, Tanesco imependekeza kufutwa kwa gharama
ya huduma kwa wateja (service Charge) na huduma ya
service line, na kuondoa gharama za fomu ya maombi
ya maunganisho ya umeme.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji
Huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ya Huduma za
Nishati na Maji (Ewura CCC), Thomas Mnunguli,
alisema katika wasilisho la shirika hilo, inaonyesha ili
kufuta gharama hizo Tanesco italazimika kukopa Sh.
Bilioni 699 ikiwa ni kukidhi mahitaji ya muda mrefu.
“Huu sio uamuzi sahihi kwa sababu mwisho wa siku
riba kubwa ya mikopo ya benki atabebeshwa mlaji,"
alisema Mnunguli.
"Mikopo ya benki inahitaji uwekezaji wa muda mrefu,
Tanesco inatakiwa ikusanye madeni yake ambayo hadi
mwishoni mwa mwaka jana lilifikia Sh. Bilioni 374.9.”
Mnunguli, ambaye ni injinia kitaaluma, alisema endapo
madeni hayo yatapunguzwa uwezekano wa bei ya
umeme kupungua kwa kiasi kikubwa zaidi ya
pendekezo la Tanesco la sasa ni mkubwa.
Aidha, walaji walipendekeza Tanesco liwakatie umeme
wadaiwa sugu ili kuwalazimisha kulipa madeni yao
ambayo yatasaidia shirika kujiendesha badala ya
kukopa.
Pia baraza hilo lililitaka shirika liweke bayana namna
litakavyolipa mkopo huo.
SOURCE: NIPASHE
 
Back
Top Bottom