Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yasema haina kisiwa cha Mchanga, inaanza kuagiza kutoka nje

Euphransia

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
937
778
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza rasmi kuwa kisiwa hicho hakina maliasili ya mchanga na hatua za kukabilaina na tishio hilo zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuruhusu mchanga kuingizwa kutoka nje ya Zanzibar na kuweka utaratibu mpya wa ugawaji.

Msimamo huo umetolewa na waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohamed wakati akiongea na watendaji na kutoa taarifa rasmi hiyo ya serikali ambapo amesema Zanzibar haina mchanga na hatua za kukabiliana na hali hiyo zimeanza ikiwa ni pamoja na kusitisha huduma hiyo siku za mapumziko na kuweka vibali na utaratibu maalum wa zamu kwa vile hali ni mbaya, na kisiwa hakina maliasili hiyo na kuwataka wananchi wabadilike ikiwa kutafuta mbinu mpya za ujenzi bila ya malighafi hiyo ya mchanga.

Mhe. Hamad Rashid ambaye ni moja ya waziri mchapakazi wa Dr Shein amesema matumizi ya maliasili hiyo ni kubwa kuliko uwezo ambapo kwa sasa unguja waanachimba tani 20,140 kwa mwezi na pemba 1522 huku katika kipindi cha miaka 10 zaidi ya tani 2.6 miloni zimechimbwa hivyo eneo lilobaki la hekta 14 halitoshi na lazima lilindwe na lipangiwe.

Msimamo huo wa serikali tayari umenza kuleta machungu yake ambapo ITV imeshuhudia gari moja la mchanga likiuzwa kwa shilingi laki moja badala ya 65,000 elfu ,huku baadhi ya wadau hao wakiwemo madereva,wachimbaji na wauzaji wakiongea na ITV katika kituo kikuu cha usambazaji cha mwanakwerekwe chenye wafanyaakazi zaidi ya 1500 wamesema uamuzi huo ni balaa na utaleta hasara kubwa na serikali ikae upya na kutafakari.

Source.ITV
 
Hii ni habari nzuri. Mimi ninamiliki mgodi wa mchanga ktk eneo la Mukuranga. Ninayo leseni ya uchimbaji na certificate ya mazingira.
Niko tayari kushirikiana na wenzetu wa Zanzibar ktk hii biashara ya mchanga. Badala ya kuagiza kutoka nje ya Tanzania.
Muhimu ni kujua logistics ya kufikisha huo mchanga Zanzibar. Aidha watahitaji kupelekewa au wataufuata huku?. Waziri anapaswa kuwa wazi kwa hili. Migodi ya mchanga iko mingi wilaya ya Mukuranga na Kisarawe, ni kujipanga tu.
 
Kufa kufaana. Badala ya kujenga bomba la kusafirishia mafuta, sasa ni zamu ya kujenga bomba la kusafirishia mchanga!
 
Kuna waziri, nimemsahau, akiwa anatetea muungano wa serikali mbili aliwahi kusema.
wanasiasa waache rohombaya wanajua kabisa kua kisiwa cha Zanzibar kila baada ya muda kinazama kwa sentimita (inchi) kadhaa hivyo kuungana na sisi ni moja ya tumaini lao juu ya hiki kisiwa, kuweni na utu.

Kwahiyo tangu zamani walijua kua kisiwa kile hua kinazama na hawakuchukua hatua, eti leo ndiyo wanakuja na huo mpango.
Watanzania hatufanyi mazingira yatuheshimu (kwa kuyaheshimu) badala yake tunangoja yatukumbe ndiyo tuanze kuyaheshimu, labda tunakua bize kula nchi mpaka tunajisahau.
 
Hii ni habari nzuri. Mimi ninamiliki mgodi wa mchanga ktk eneo la Mukuranga. Ninayo leseni ya uchimbaji na certificate ya mazingira.
Niko tayari kushirikiana na wenzetu wa Zanzibar ktk hii biashara ya mchanga. Badala ya kuagiza kutoka nje ya Tanzania.
Muhimu ni kujua logistics ya kufikisha huo mchanga Zanzibar. Aidha watahitaji kupelekewa au wataufuata huku?. Waziri anapaswa kuwa wazi kwa hili. Migodi ya mchanga iko mingi wilaya ya Mukuranga na Kisarawe, ni kujipanga tu.
Huko ndiko kunaichangamkia fursa!!
 
Katika pitia pitia ya magazeti nimekutana na hii ya SMZ kuagiza mchanga nje ya nchi...

Wakuu imekaaje hii.
90c3518cbf1c0d8ca9829b81ca943e7c.jpg
 
Back
Top Bottom