Serikali ya Lowassa na UKAWA ingefanya haya ili kutimiza ahadi zake!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Igwe wanaJF.

Katika tathmini yangu ya miezi sita ya Utawala wa John Magufuli (PhD) akifanya mambo ambayo yamestaajabisha,kuibua uozo,kujenga nidhamu na kurekebisha makosa bila kujali watu hasa wapinzani watatafsiri vipi.Nimefuatilia kauli za Lowassa,KUB Mbowe na wana UKAWA na kwa hakika wengi mtakubaliana nami kuwa serikali ya Lowassa ingefanya yafuatayo;

1.Kwenye Elimu,nisingeshangaa Lowassa kutanua goli ili kuongeza idadi ya "wasomi" ,plagiarism, kama alivyodesa nzima nzima kauli mbiu ya ELIMU,ELIMU,ELIMU alidesa kutokwa kwa Tonny Blair (1996) "Ask me my three main priorities for government,and I tell you: Educatio,Education,Education"..Tonny Blair alimaanisha Kusimamia sera ya Elimu UK kuanzia vidudu hadi Chuo kikuu ili kuzalisha wanafunzi bora duniani,kurudisha hadhi ya vyuo vya UK katika ubora duniani.Alipoingia madarakani alidhibiti udahili wa hovyo vyuoni hasa kwa wanafunzi wanaotoka nje ya UK nk.Angependa kila mwanafunzi "afaulu" hasa ukifuatilia kwa sasa bavicha wamegeuka kuwa watetezi kwenye kila uozo.

2.UCHUMI
Hapa ndipo tungekoma,sera ya Lowassa na Chadema ilikuwa ni kutengeneza mamilionea kama Mengi na Bakhresa 20,000.Ingekuwa ni serikali ya kila mbuzi ale urefu wa kamba yake.Chadema kwa sasa wamepewa jukumu la kutetea wabadhirifu,wakwepa kodi,wauza unga nk.Mara kwa mara Lowasa,Mbowe na Wafuasi wa Chadema wamekuwa wakisema wahalifu wanakamatwa sababu ni wafuasi wa Chadema bila kutoa ushahidi ni jinsi gani hawahusiki.Tundu Lissu alidiriki kuwashauri watu hao waende mahakamani na yupo upande wao.

3.Nishati na Teknolojia.

Hili eneo ndilo haswa lilikuwa lengo kuu la UKAWA.Leo wataalamu kutoka Thailand wangekuwa wameshalipwa hela ili kutengeneza "Mvua".Kwenye eneo la nishati huyu jamaa ndiye bingwa wa mikataba ya fasta fasta na maswahiba wake kina Karamagi wazee wa kutembea na mihuri ya serikali hakika nchi ingrshachoka sasa hivi.Tumshukuru Mungu aliyeingilia hii vita.

4.Afya.
Dah hapa kama alivyokuwa anaenda kliniki ya macho ujerumani kwa sasa watu wa hali ya chini bajeti ya afya ingetumika kutibu viongozi ulaya.Tokea JPM kaingia Ikulu hamna kiongozi alienda check up majuu,Sumaye alitibiwa Muhimbili.Wabunge hamna aliyepelekwa India kama ilivyozoeleka.

5.Uchumi
Hapa kama tumjuavyo mzee angepiga yeye na genge lake kisha kuhadaa wananchi kupitia harambee za mfululizo kwenye makanisa,miskiti,bodaboda,Saccos nk ili kujenga dhana ya "mtakapoyumba kiuchumi tutagawana vya kwangu"..kuunda makundi ya vijana nchi nzima wanaolipwa ili kujenga ushawishi hii ni 4U na Bavicha maslahi.

6.Ufisadi.
Mtu yeyote ambaye angepinga ufisadi ingeanzishwa mahakama maalum kufunga watu wanaopinga ufisadi kwani wanafuatilia maisha ya watu.Katika falsafa ya "haki za binadamu" Chadema wanaamini katika kutajirika kwa mbinu yoyote "hakuna kufufua makaburi",piga hela sepa.

Nimeanisha maeneo machache,ninaamini kwa maoni yenu mengi mmegundua kutokana na matamshi ya Wanachadema.

Nauliza tu vipi Bungeni Ukawa bado wamesusa?

Tujadili kwa kuzingatia kanuni za JF tusitolewe nje.
 
navyomwona mke wa lowassa mahakamani akifatilia kesi ya mkwe wake najiuliza mme wake angekuwa madarakani kesi kama hizo zingekuwa zinamalizwa chumbani mwao hivi unampelekaje mahakamani mme wa mwanao hizo pesa waambie walete mgao huku sehemu zote nyeti zingeshikwa na walewale wapiga dili
 
Tunachokieleza hapa ni hakika.Habari za Uhakika ni kuwa Mwanahalisionline wamgomea Mbowe na Chadema kuondoa habari zilizotoa tuhuma za Lowassa akiwa CCM,ikumbukwe Chadema walishanyofoa kwa hiyari orodha ya mafisadi.
 
Alisema pia angeanzisha benki ya bodaboda.
Eti ukienda tu benki ukiwa unaendesha bodaboda bila kujali inamilikiwa na nani unachotewa pesa unasepa.
Nashukuru Mungu kwa kutuepusha na Lowassa.
 
Back
Top Bottom