Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,158
- 3,109
Kada wa CHADEMA, Godbless Lema akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni amewataka wananchi kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, licha ya changamoto za ukiukwaji wa taratibu na sheria.
Soma pia: Lema wa CHADEMA afichua madudu mazito kwenye zoezi la uandikishwaji wa wananchi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Asema Serikali inaiba Uchaguzi
Lema amedokeza kuwa kuna umuhimu wa kila mwananchi kujisajili ili iwe rahisi kubaini wizi wa kura iwapo utatokea.
"Nilitoa video kama ya tangazo ya kuwahamasiha nyinyi wananchi, muende mkajiandikishe na nilisema maneno yafuatayo: pamoja na figisufigisu na ukiukwaji wa taratibu na sheria na kanuni lakini nendeni mkajiandikishe (Kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa) ili wakishinda kwa wizi, tujue wameshinda kwa wizi"
Aliongeza kwa kusema:
"Hii taarifa ninaitoa kwa wananchi wote nchi nzima hususan kanda ya Kaskazini ambapo mimi ni mwenyekiti wake (CHADEMA). Wananchi wa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha, kwa siku sita zilizobaki, pamoja na hali yote ambayo tunaiona nendeni mkajiandikishe kwa wingi, ili wakiiba kura tujue wameiba kura, ni muhimu sana kila mtu akajiandikisha"