Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wa dola milioni 207.3 sawa Tsh bilioni 466.4

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.

Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.

Baadhi ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.

Dkt. Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani ya shilingi bilioni 77,

Mradi mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.

IMG_1538.JPG
IMG_1563.JPG
 
Asanteni sana KUWAIT
Wanakopa Marekani ije kuwa nyie bana
Kopaaaaaaa, na bado tunakopesheka sana tu.
My the way, nasikia kuna gesi asilia imepatikana huko Malinyi, Morogoro. Tutafute mtu tumkopeshe gesi yetu atupe mkwanja siye tufanye maendeleo
 
Katika kipindi cha miaka 40 Kuwait imetupa mkopo wa shilingi bilioni 600, ndani ya mwaka moja wanatupa mkopo wa shilingi bilioni 460! Jamaa kaamua kutuuza mzima mzima aisee. Sijui yeye anapanga kuamia sayari gani!!!?
 
hila kikwete katika ushawishi alikuwa vizuri billion km hizo husikii mkopo tungeambiwa ni msaada wa maendeleo.
 
Mijitu inakopa tu, mwanzo mwisho. Kazi yao imebaki

KUKOPA
KUHONGA WAPINZANI
KURUDIA CHAGUZI
KUCHUKUA WAKE ZA WATU
KUPIGA WATU RISASI
ndio vipaeumbele vyao hvyo mkuu"" usi washangae sana""
halafu kwenye malipo wanategemea kodi na rasilimali zetu. """ wananchi wa nchi hii sijui tumerogwa....!!?
 
Asanteni sana KUWAIT
Wanakopa Marekani ije kuwa nyie bana
Kopaaaaaaa, na bado tunakopesheka sana tu.
My the way, nasikia kuna gesi asilia imepatikana huko Malinyi, Morogoro. Tutafute mtu tumkopeshe gesi yetu atupe mkwanja siye tufanye maendeleo
hahaaa hii scenario imejaa uchochezi mtupu ...wacha tukope tu ..kwani kitu gani...hahaa
 
Mkopo wa masharti na fuu huo ....tukishindwa kulipa .nchi si ina tembo .twiga .simba .duma..
fisi .na vyura wa kihansi ....achilia mbali madini yaliyopo na gesi ” tutaviweka dhamana hta hvyo aisee""""
 
Natamani kujua sahv deni letu la Taifa limefikia kiasi gani?

Ova
 
Hata marekani wanakopa
And that is the problem with us...the tragedy of comparing ourselves with United States of America, that's a demonstration and mark of inferiority complex...the assumption that what America does is the be all and all... it is wrong...tubadilike..si tuliambiwa tuna hela ya kutosha kwa nn tukope
 
Back
Top Bottom