ibr_the_brain
Member
- Jun 28, 2015
- 26
- 21
Ukweli ulio wazi ambao watu wengi wamekuwa wakisifu na kupongeza vitu ambavyo havina maana kubwa kwa mwananchi wa kawaida.
ZIARA ZA KUSTUKIZA
Je, ni ziara gani ya rais ya rais imekuwa ya kustukiza? Kila ziara naona yuko na waandishi wa habari ni nini anachokistukiza? Kuweni macho tunatengenezwa tuamini vitu ambavyo vimepambwa na waandishi wa habari. Wakati kufanya kazi jukumu lao waandishi wa habari wa nini kila kona? Mi ninachoamini hata kibaya kikipambwa kitaonekana kizuri.
SUALA LA ZANZIBAR
Jana jumapili siku ya Uchaguzi Zanzibar mimi kama mwanaharakati ambae sifungamani na chama chochote nimeumia sana kwanini watanzania wanakosa haki yao ya kimsingi kuwalazimisha kile watakacho wao? Tunaomba swala hili liangaliwe upya tume zetu sio huru na haki kila mtu analijua hilo.
Rais JM alisema ni rais wa wanyonge, hivi ni wanyonge wapi anao wazungumzia, kufukuza vigogo haitoshi maana hata wakifukuzwa wanaenda jela miezi miwili wanarudi mtaani kwa kisingizio cha kifungo cha nje kama Yona na Mramba. Wanyonge wa Zanzibar hawajapiga kura, hili nalo sawa? Umeme kukatika nchi nzima? Usanii mwingi!
MIKATABA MIBOVU
Hili linatutesa watanzania wote wakati wa kampeni alisema atalishughulikia mpaka sasa hatuoni kinachoendelea zaidi ya maneno mengi bila ya vitendo.
UTENDAJI KAZI
Hatuwezi kusifia kila jambo, kufanya kazi ni wajibu wa kila mtu sio kila kazi anayoifanya rais tuijue apana afanye kazi kama kazi mbona sisi tunafanya kazi atuzunguki na waandishi wa habari?
Maana naona watanzania tunatengenezwa kisaikolojia tuamini kufukuza watu na kukusanya pesa ndio maendeleo wakati mengi yanayotuzunguka ni kero kwetu; barabara mbovu *chini ya kiwango* ,umeme shida ,maji ni tatizo pesa kwa mwananchi wa chini zinakusanywa kama kodi na kurudi taratibu kwenye mzunguko.
TUWE MACHO
Kama kila kazi tutaenda kwa camera, itafika siku bila camera kazi aitafanyika.
Naomba kuwasilisha..