Serikali ya Kenya yaomba kuajiri madaktari Tanzania

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Serikali ya Kenya imeiomba Tanzania kuiruhusu kuajiri madaktari kutoka nchini humo ili kujaza nafasi ya madaktari walioingia kwenye mgomo kwa zaidi ya siku 90 hadi sasa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amethibitisha kupokea ombi hilo la Serikali ya Kenya. Hata hivyo, hakutaka kutoa ufafanuzi zaidi.
“Ndio… lakini tafadhali usiniulize maswali zaidi,” Waziri Ummy anakaririwa na The Citizen.
Hivi karibuni, Serikali ya Kenya ilitangaza mpango wa kuwaajiri madaktari kutoka Tanzania, Ethiopia na Cuba kwa lengo la kuziba pengo la madaktari walioingia katika mgomo nchini humo.
Hata hivyo, Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT) kupitia kwa Mwenyekiti wake mteule, Dkt. Elisha Osati jana kilieleza kuwa hakiungi mkono ombi la Serikali ya Kenya katika kipindi hiki ambacho madaktari wa nchi hiyo wako kwenye mgomo.
“MAT haiungi mkono mpango wa Serikali ya Kenya kuwaajili madaktari wa Tanzania. Labda kama ombi hili litafanyika baada ya mgomo kuisha,” Dkt. Osati aliandika kupitia mtandao wa Twitter.
Ombi hilo limekuja ikiwa ni siku chache baada ya MAT kuiomba Serikali kuwaajiri madaktari kwani kuna zaidi ya madaktari 1500 wapya waliopewa leseni lakini bado hawajaajiriwa.
Madaktari wa Kenya wameingia kwenye mgomo wakidai ongezeko la mshahara wa kima cha chini hadi shilingi milioni 9,700,000 za Tanzania, kiasi ambacho Serikali ya nchi hiyo imesema haiwezi kumudu.
by dar24
 
Jinsi wakenya walivyo na msimamo....kiusalama ni risk labda kama watawapa ulinzi hao madaktari.
 
Pamoja kuwa ni fursa nzuri kwa madaktari ambao hawana hawajapata ajira, mazingira yaliyopo nchini Kenya si muafaka. Nafikiri ni vyema wajiepushe kuwa kikwazo cha maongezi kati ya serikali ya Kenya na madaktari waliogom. Madai ya madakitari waliogoma Kenya ni ya msingi haswa ukizingatia kazi wanayofanya ikilinganishwa na sekta nyingine, haswa siasa. Mbali na ujira, madaktari hao pia wanadai kuboreshwa kwa mazingira ya utoaji wa huduma za afya kwa ujumla mbali na picha inayojengwa kwamba wanadai maslahi binafsi. Endapo madaktari kutoka nje watakubari kuajiriwa katika mazingira haya, watawanyima madaktari wa na Wakenya kwa ujumla fursa ya kuwabana wanasiasa kuhakikisha wanaboresha mazingira ya utoaji huduma za afya na za jamii kwa ujumla. Pia kwa kufanya hivyo, itakuwa ni kuwapa wanasiasa ushindi wa kujari zaidi maslahi yao na kukanyaga ya wengine richa ya uzito wa kazi husika. Kama madaktari kutoka nje watakubari kwenda kufanya kazi katika mazingira yaliopo Kenya hivi sasa, basi tutegemee kile kinachotokea Afrika ya Kusini kwani itakuwa tunapandikiza mbegu za chuki dhidi ya wageni.
 
Watawapata wengi na hata waziada watakao taka kujipeleka wenyewe watawapata,kwa kuwa madaktari wengi wamevunjika moyo kufanya kazi nchini.

Tatizo ni usalama wao utakuwaje watakapokuwa nchini Kenya kwa kuwa wanakwenda kuchukua nafasi za watu waliotimuliwa kazi.
 
Waende tu sisi tumesitsha kuajiri tunafanya uhakiki kwanza
 
Back
Top Bottom