Serikali ya Kenya inasema Kaunti zaidi ya 10 nchini humo zinakabiliwa na baa la njaa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Serikali ya Kenya inasema Kaunti zaidi ya 10 nchini humo zinakabiliwa na baa la njaa kwa sababu ya ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua.

Wakenya zaidi wameendelea kuathirika na baa la njaa haswa katika Kaunti zilizoko maeneo yenye ukame kama vile Turkana ambapo vifo kutokana na jinamizi hilo vimeripotiwa, kwa mujibu wa mashahidi.

Hata hivyo Naibu rais William Ruto amesema, serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa katika Kaunti ya Turkana iliyoathiriwa zaidi, na kukanusha ripoti kuwa watu tisa wamepoteza maisha kwa sababu ya njaa.

Kwa upande wake Waziri Eugene Wamalwa amesisitiza kwamba Kenya ina chakula cha kutosha ambacho kitasambazwa katika maeneo yaliyoathirika.
 
The big tragedy worst than hunger itself is how to get there, Hapa ndio mahali hesabu zote kwamba Kenya imeendelea kimiundombinu zinakataa, kufika hayo maeneo kupeleka chakula cha msaada ni sawa na kutoka Jupiter kwenda one of the asteroids.

Inaweza kuchukua zaidi ya week kuwapatia msaada hao watu
 
Serikali ya Kenya inasema Kaunti zaidi ya 10 nchini humo zinakabiliwa na baa la njaa kwa sababu ya ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua.

Wakenya zaidi wameendelea kuathirika na baa la njaa haswa katika Kaunti zilizoko maeneo yenye ukame kama vile Turkana ambapo vifo kutokana na jinamizi hilo vimeripotiwa, kwa mujibu wa mashahidi.

Hata hivyo Naibu rais William Ruto amesema, serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa katika Kaunti ya Turkana iliyoathiriwa zaidi, na kukanusha ripoti kuwa watu tisa wamepoteza maisha kwa sababu ya njaa.

Kwa upande wake Waziri Eugene Wamalwa amesisitiza kwamba Kenya ina chakula cha kutosha ambacho kitasambazwa katika maeneo yaliyoathirika.
Harafu wakenya wa jf wanasema wanavimbiwa kila siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom