Serikali ya Congo yazuia uuzaji madini Ng'ambo

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Serikali ya Congo yazuia uuzaji madini Ng'ambo

Kampuni kumi na sita za kuchimba madini zimepigwa marufuku ya kuuza bidhaa zao katika nchi ya ngambo, na utawala wa mkoa wa kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wa Katanga.

Maafisa wa serikali wanasema kampuni hizo, zimekiuka masharti waliowekewa ya kusaidia na kuimarisha shughuli za kilimo katika maeneo wanayochimba madini.

Mwaka uliopita mkuu wa mkoa wa katanga, Moise Katumbi, aliagiza kampuni hizo zipande hecta mia tano za mpunga, ili kuwalisha wakaazi wa mkoa wake na kupunguza viwango vya chakula wanavyoagiza kutoka mataifa ya ngambo.

Miongoni mwa kampuni zilizoadhibiwa ni pamoja na kampuni kumi kutoka uchina, na zingine kutoka Ubelgiji na Canada. Kampuni hizo huchimba madini ya Cobalt ambayo inapatikana na kiasi kikubwa nchini Congo.

SOURCE: BBC

Swali yangu: Je sisi tuna uwezo wa kuziadhibu kampuni ambazo bado zina wanyanyasa wananchi waishio jirani na migodi ambao licha ya chakula hawana hata kisima au bomba la maji ya kutumia? mradi ambao ni mishahara ya miezi miwili ya wakurugenzi wawili wazungu.
 
Serikali ya Congo yazuia uuzaji madini Ng'ambo

Swali yangu: Je sisi tuna uwezo wa kuziadhibu kampuni ambazo bado zina wanyanyasa wananchi waishio jirani na migodi ambao licha ya chakula hawana hata kisima au bomba la maji ya kutumia? mradi ambao ni mishahara ya miezi miwili ya wakurugenzi wawili wazungu.
Subutu!!!
 
Back
Top Bottom