Serikali ya CCM na Utitiri wa Vyeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya CCM na Utitiri wa Vyeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by yutong, Jul 15, 2011.

 1. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mfumo uliopo wa sasa wa CCM unastahili kufanyiwa marekebisho makubwa kwani ni mzigo mkubwa kwa watzanzania na hasa ukizingatia unatumia kodi za watz ambao ndo kwanza hawana maji, hawana umeme, hawana shule za uhakika kwa ajili ya watoto wao.

  Hebu nianze na Mkoa wa Dar es Salaam labda; viongozi hawa wote tija iko wapi?
  1. Mkuu wa Mkoa (RC)
  2. Katibu tawala wa Mkoa (RAS)
  3. Meya wa Jiji
  4. Mkurugenzi wa Jiji
  5. Wakuu wa wilaya watatu
  5. Makatibu tawala wa wilaya watatu (MaDAS)
  6. Mameya wa Manispaa watatu
  7. Wakurugenzi wa Manispaa watatu

  sasa huo utitiri wa viongozi hapo juu tujiulize je unaendana na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam? labda mniambie nini wajibu wa kila kiongozi hapo juu? lakini tunashuhudia mji uko ovyo ovyo. Pia ukiangalia hapo juu kila aliyetajwa hapo ana Shangingi lake la kumtoa nyumbani kwenda kazini. Kweli mtu ambaye yuko Dar es Salaam anahitaji gari kubwa namna hiyo kumtoa nyumbani kwenda ofisini na kumrudisha nyumbani kila siku? Tujiulize hapo?

  Pia kuna utitiri wa taasisi na mashirika ambayo hayana Tija kwa mfano ktk Tanesco kuna kitengo cha Umeme vijijini, lakini kuna REA nk? Kazi hasa ya REA sasa ninini? Je, Toka REA ianze imeshafanikiwa kuweka umeme vijiji vingapi? Kuna TIRDO, TPDC, TIPPER, nk. Pia kuna EWURA, SUMATRA, hebu tujiulize haya mashirika hasa yanachangia ama yameleta mabadiliko gani ya msingi kwa watz zaidi ya kuongeza gharama kwa watz? maana kila unaponunua umeme unakatwa pcntg kwenda Ewura, ukinunua petrol unakatwa pcntg kwenda ewura, maji unakatwa pcntg kwenda ewura, sasa tujiulize kwanza katika hela wanayopata ewura inakwenda wapi? je ni wao kujilipa tu na safari zisizo za msingi, je wizara kama wizari haiwezi kusimamia? Kuna NHC, kuna TBA nk tofauti ya NHC na TBA ni nini? je kazi za shirika moja wapo haziwezi fanywa na shirika moja ama wizara? Hii yote ni matumizi mabaya ya kodi za watz, badala ya kuongeza shule zaidi, hospitali zaidi CCM wao wameamua kujaza mashirika mengi zaidi yasiyo na Tija kwa watz na ambayo nimzigo kwa serikali. Kunaidara mbalimbali kila wizara ambazo zingeweza kusimamia shughuli zote hizo kwa gharama nafuu. Mashirika yaundwe pale ambapo kunaulzima wa kufanya hivyo na wakati fula yawe ya muda ili kutimiza lengo fulani.

  Hivyo basi inawezekana CCM wameunda mashirika yote hayo ili kuweka mitego ya mapato yao na njia ya kuiba pesa ya watz. Kwa mfano mashirika ya hifadhi za jamii kwa nini yawe mengi hivyo wakati kazi zao nimoja? Kama hivyo ndivyo kwa nini Shirika la Bima ya Afya ni moja kwa wafanyakazi wote? watz fumbueni macho CCM wana mbinu nyingi kutuibia. sasa tuseme basi imefika mwisho. katika taifa masikini kama letu nilitegemea kuona serikali inajenga shule nyingi toka za nasale mpaka vyuo vikuu na hospitali za kutosha. wansema wananchi wachangie ujenzi wa zahanati/shule mbona kununua magari hawasemi tuchangie? je hizo hela wanazipata wapi? kwa nini zisingetumika kujenga shule/zahanati? Serikali ya CCM ni wanafiki ambao wanawadanganya wananchi kuwa serikali haina hela wakati wao wakiishi maisha ya kifahari nakuendesha magari ya kifahari ambayo hata waliotengeneza hawayatumii kukwepa gharama.

  Natumaini mmenielewa na kama bado mtu unaona CCM iko ok basi utakuwa unamtindio wa ubongo.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wanamagamba watakuambia mchonganishi kwa kutoboa siri zao
   
 3. Researcher

  Researcher Senior Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asante kwa mada yako nzuri ingawa siwezi kuiunga mkono moja kwa moja mifano yako kwamba michango ya taasisi ulizozitaja ni sifuri..

  Pengine hoja ya msingi katika mada yako ni mtazamo wa kifikra au kisera tulionao juu ya tija na ufanisi wa serikali na taasisi zake;
  1) Kwamba tukiongeza idadi ya taasisi, wilaya, mikoa au watumishi bila kuangalia uwajibikaji tutaimarisha ufanisi wa serikali.
  2) Kwamba kwa kufanya hivyo vileville tutafikisha huduma karibu zaidi na wananchi na vilevile tutaongeza ajira.

  Inabidi tuanze kufuta mtazamo huu.Binafsi napendekeza kwamba:-
  1)Serikali ianzishe perfomance based budgeting kuhakikisha uwajibikaji kuanzia ngazi ya mtumishi mmoja mmoja.
  2) Serikali ianze kuangalia taasisi zenye majukumu yanayofanana au kuingiliana na kuziunganisha ili kupunguza gharama (Mfano TIRDO na TEMDO, TFDA na TBS, Makamu wa Rais mazingira na NEMC na mengine meeengi)
  3) Serikali ianze kuondokana na dhana kwamba kuanzisha mikoa na wilaya mpya ni njia pekee na badala yake iimarishe miundo mbinu na kutumia teknolojia kuboresha ufanisi wa tawala za mikoa na serikali za mitaa.

  4) Ni kweli tunahitaji ajira zaidi, lakini tuangalie kwa mapana na marefu manufaa na hasara za kuwa na watumishi au mashirika mengi yasiyofanya kazi kwa tija.
   
 4. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kaka hapa sikuwa na maana kwamba kazi za haya mashirika ni sufuri kabisa, ila tunaangalia efficiency ya haya mashirika. Kwa mfano mi nahoji shirika kama EWURA lina mchango gani kwa taifa letu? Labda uweke hapa wazi kazi za kila shirika na mafanikio yake sio kuzungumza theoretically. Tusifikirie kuongeza utitiri wa ajira zisizokuwa na tija kwa taifa badala yake tulrnge ajira zenye kukuza uchumi wa taifa letu kama viwanda, kilimo, usafirishaji nk na si eti kuongeza utitiri wa vyeo na mashirika huku ukijidanganya unaongeza ajira ni upuuzi huu
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena kitaaalamu zaidi. Ni kweli muundo wa Serikali inabidi uangaliwe upya na kuunganisha baadhi ya idara, vyeo, nk.
   
 6. Mr. Mwalu

  Mr. Mwalu JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Nakumbuka mhe raisi siku anarudisha fomu ya kugombea urais pale lumumba, aliwahutubia na kuwaomba walioshindwa kwenye uteuzi wa wagombea, wasikimbie atawagaia mavyeo! Kwamba mavyeo yapo mengi
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Dawa yao Katiba Mpya tu basi. Ikija katiba mpya iweke vyeo na sio kila akija Rais anajiundia vyeo ambavyo hata havieleweki ili mradi tu kuwa accommodate watu fulani!!
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tatizo kubwa la sisi nchi maskini bajeti yote inaishia kwenye mambo ya utawala tu...
   
Loading...