Serikali ya CCM kuwanyima wananchi machaguo ni dharau isiyomithilika

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,615
51,547
Hawa watu wamefikia kilele cha kiburi, jeuri na dharau ya hali ya juu mno isiyo na kifani!

Wamefikia hatua ya kuona wananchi wa Tanzania ni wapuuzi, wajinga na hawastahili kuwa na machaguo yao kwa utashi wao huru ya kuchagua viongozi wawatakao isipokuwa tu wale wanaowaimpose wao.

Kusema kweli hiki ni kiburi kilichovuka mipaka, ni Udhalimu usiomithilika. Wamevuka mipaka hawa!!

Hizi tabia za kutoheshimu chaguzi zina mizizi mirefu katika nchi hii, hii mbegu hii ambayo leo imeota na kuanza kutoa matunda yake ilianza zamani, ilianza toka mwaka 1995 huko Zenji, na kwa bahati mbaya Muasisi alikuwepo na akabariki mambo yale.

Waliofuata nao wakaanza kutembea katika njia ileile, maana kama Muasisi kabariki kupindua matakwa ya wananchi then kwani nao kuna ubaya gani kutoheshimu matakwa hayo pindi wakiamua kutoheshimu?

Ila tofauti ya hawa na Muasisi ni moja, Muasisi alikuwa na haya, alikuwa na aibu, roho yake ilimsuta kwa kitendo kile, moyo wake ulivia baada ya kushiriki jambo lile. Akaamua kupendekeza serikali ya mseto kule Zenji, kwamba kwa kuwa wewe uliyeshinda umeshinda kwa margini ndogo sana basi kubali tu kuwa hata huyu uliyemshinda anapendwa na wananchi, kwa hiyo undeni serikali ya pamoja!. Muasisi akajibiwa na komandoo kuwa ushindi ni ushindi tu hata kama ni wa kura moja!!. Muasisi akakosa kauli maana ni yeye aliyeshiriki huyo mshindi wa kura moja kupata huo ushindi!

Mbegu mbaya ilipandwa hapo, kisha ikaendelea kukua, matokeo yake yakaanza kutokea katika chaguzi zilizofuata huko Zenji na mwishowe yaliyotokea mwaka 2015 sote tukayaona, dunia ikayaona lakini hawa mabwana wakubwa hawajali, hawaoni haya tena na kiufupi hawana hofu ya mwananchi yeyote kwa sababu kwao ridhaa ya umma siyo factor muhimu tena ya wao kukaaa madarakani.

Jakaya alibariki uhuni uliotokea Zenji mwaka 2015, akiamini kwa kufanya hivyo anaitendea CCM yaliyo mema. Akabariki dhulma za wananchi wa Zenji kwa moyo wake na akili yake.

Leo hii hata haya yanayotokea Tanganyika leo, unadhani kuna mwana CCM anayekwazika, anayeumia kuwa tunawatendea wananchi wa nchi hii dhulma kwa kuwalazimishia viongozi?

Kiufupi CCM imefikia kilele cha kutoogopa umma, na ndiyo maana haiheshimu machaguo ya wananchi.

Kinachofuata baada ya hapo ni umma wenyewe kwa njia zozote zile zilizo effective kupitia kwa watu wabishi na walio "enlightened" miongoni mwao, wasiokubali dharau kufanya jambo litakalorudisha nidhamu ya watawala kwa wananchi!, Ni heri watawala wakastuka la sivyo wasije baadae kupigwa na mshangao itakapotokea jambo kama hilo wasijue la kufanya na wasijue imekuwajekuwaje!.

Watawala wajue wakiondoa haki za wananchi kwa nguvu basi wapo wananchi watazidai kwa nguvu

Wakiondoa kwa hila dhana nzima ya wananchi kujitawala kwa ridhaa yao, basi wapo wananchi watatumia nao hila kurudisha mamlaka yao mikononi mwao

Si vyema watawala kujiinua kwa Kibri, dharau na Jeuri mbele ya umma namna hii. Haya ni matusi makubwa mno na umma kamwe hauwezi kukubali!
 
Tatizo lipo kwa sisi wananchi hatuna shukrani na uelewa kwa anayofanya JPM .Yasemekana tafiti na hata mrejesho viongozi serikali vijiji na mitaa kikao ikulu, idadi kubwa Watz bado hawamuelewi JPM, ilimpa huzuni sana mkuu. Hivyo yakatolewa maelekezo mahususi ushindi 100% iwe jua ama mvua.
 
Vichaa wamepewa nchi waongoze, tukivuna matunda yanayoendana na ukichaa tusilalamike.
 
Tatizo lipo kwa sisi wananchi hatuna shukrani na uelewa kwa anayofanya JPM .Yasemekana tafiti na hata mrejesho viongozi serikali vijiji na mitaa kikao ikulu, idadi kubwa Watz bado hawamuelewi JPM, ilimpa huzuni sana mkuu. Hivyo yakatolewa maelekezo mahususi ushindi 100% iwe jua ama mvua.

Sasa kwenye nchi yenye uongozi makini ilitakiwa afanye mambo ya kuwagusa wananchi moja kwa moja kama vile kusolve kwa nguvu zote ishu za Maji, Kilimo, Uvuvi, Ajira kwa watoto wao, Elimu bora siyo bora elimu.
Alitakiwa adeal na NEEDS za wananchi kwa nguvu nyingi zaidi kuliko jinsi anavyodeal na WANTS
Maji ni Need wakati ndege ni WANT
Angefanya hayo watu wangemuelewa zaidi kuliko propaganda za Tunatekeleza, Unatekeleza nini?, Eti nimenunua Ndege, sasa hizo ndege zinamgusa vipi raia wa chini huku moja kwa moja kwenye ishu zake za mahitaji ya msingi?
 
Wananchi huenda wanaichukia CCM kuliko wanavyomchukia Magufuli.

Pamoja na mapungufu mengi ya kimtazamo aliyonayo Magufuli, endapo atawezesha kupatikana katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, na mifumo inayofanya kazi kwa weledi bila kutegemea maagizo, atamzidi baba wa taifa Mwl Nyerere.
 
Malcolm X alisema; Watawala wa namna hiyo ili wakuelewe inabidi uzungumze lugha wanayoielewa wao, nayo ni lugha ya kuitetea haki yako by any means necessary. Ukizungumza lugha nyengine hawatokuelewa.

Kwa sababu mtu akishauvaa ununda lugha ya kistaarabu haielewi. Ukimuendea kistaarabu anakuona wewe ni bwege; ili akuelewe na muelewane nawe muendee kinunda kwa gharama ya namna yoyote ile hata kama atakudhuru lakini ataingiwa na hofu juu yako! Ujinga ujinga wa kipunguani hatokuletea.
 
Back
Top Bottom