Ukweli ni kuwa maliasili sio mali za wananchi. Wanasiasa wanaamini mali ya wananchi ni zile artificial kama nyumba, gari n.k

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
22,543
54,449
Kwema Wakuu!

Weekend hii nilikuwa na mzee mmoja mserikali àliyestaafu mambo ya uongozi. Katika mazungumzo yetu tukajikuta katika mjadala mkali kuhusu maliasili na rasilimali za wananchi.

Nikamwambia madini, maziwa, Gesi wanyama na maliasili zingine mali za wananchi wa taifa hili. Mzee yule akatabasamu kisha akaniambia
"Taikon nakujua kwa ubishi wako lakini nisikie, mwananchi hamiliki Maliasili. Maliasili sio mali ya wananchi isipokuwa mali za wanasiasa, watawala kwa kile kiitwacho serikali"

" Kitu pekee ambacho mwananchi anaweza kumiliki ni nyumba yake,gari na mambo yote yanayoundwa na wanadamu. Hayo ni yake na nidhuluma kuyachukua kutoka kwake. Ikitokea unayachukua lazima umpe fidia kwa sababu ni yake"

"Lakini hakunaga dhambi kwa watawala kuchukua au kutumia maliasili vile watakavyo. Kwa sababu maliasili ni mali halali ya watawala na wanasiasa"

Mwisho wa kunukuu!

Sasa Taikon kwa ubishi wangu niliachana na yule mzee kwa kinyongo baada ya kunichana. Ingawaje ni rafiki yangu lakini hoja yake hii imenipa mtazamo mpya.

Sasa nimelileta huku tujadili.

Je ni kweli Maliasili sio mali za wananchi. Bali mali za watawala au wanasiasa kwa jina lao waliitalo serikali?
Yaani bahari, madini, gesi, mbuga, maziwa,ardhi miongoni mwa maliasili zingine.

Kwenu wanazengo.

Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kaka mbona hii iko wazi kabisa kwa mifano halisi ambayo tunaiona.

Mfano mmoja rahisi kabisa ni kiwanja chako ulichonunua na kujenga nyumba. Ukisoma hati utaona pale kiwanja umepangishwa na serikali na unatakiwa kukilipia, meaning sio chako.

Labda tunaposema ni mali za wananchi ni kwa sababu serikali by definition sio mali ya mtu mmoja ila ni kundi la watu walio na mamlaka ya kutawala nchi au wizara; Kama vile wizara ya ardhi inamamlaka ya kusimamia ardhi na imekabidhiwa. Japo inaumiza ila ndio kamfumo ambako dunia/watabe wa zamani waliweka ili kuweza kucontrol binadamu.
 
Ni mfumo wa hovyo sn
 
Chimbuko la ukoloni ni ubepari. Ukoloni uliingia kwa hila na harakati za kujitoa kwenye ukoloni hazikufanyika kwa ukamilifu wake. Ukoloni bado upo hadi leo kwani ulihamishiwa kwenye kitu kinachoitwa sasa Serikali ambacho ndicho kitalu cha wanasiasa.
Kimsingi hatujapata uhuru kamili bado, tunatakiwa kuendeleza mapambano kudai uhuru tukianza na katiba mpya itakayoweka bayana tafsiri ya Taifa hili na kuwa, Ardhi na rasilimali zake zote ni mali ya wananchi na sio Serikali wala Rais.
 
Wananchi wa kawaida wao wàtakuambia wapo huru
 
Kaka mbona hii iko wazi kabisa kwa mifano halisi ambayo tunaiona.

Mfano mmoja rahisi kabisa ni kiwanja chako ulichonunua na kujenga nyumba. Ukisoma hati utaona pale kiwanja umepangishwa na serikali na unatakiwa kukilipia, meaning sio chako.

Labda tunaposema ni mali za wananchi ni kwa sababu serikali by definition sio mali ya mtu mmoja ila ni kundi la watu walio na mamlaka ya kutawala nchi au wizara; Kama vile wizara ya ardhi inamamlaka ya kusimamia ardhi na imekabidhiwa. Japo inaumiza ila ndio kamfumo ambako dunia/watabe wa zamani waliweka ili kuweza kucontrol binadamu.

Hatari sana
 
Ila hawa walafi wa sasa wamezidi, MUNGU anyooshe mkono wake atupiganie.
 
Back
Top Bottom