Serikali ya CCM isiwatume wajinga katika mambo muhimu

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Mwaka 2019 nilikishauri CHAMA changu-CCM kuacha kuwatumia watu wajinga katika mambo makubwa na ya muhimu. Niliwaambia, kazi aliyopewa Cyprian Musiba ni kazi nzuri na ya muhimu lakini kwa sababu imepewa mtu mjinga itaharibiwa vibaya na kugeuka sumu. Kazi ya kukitenganisha Chama na mtandao wa mabepari ilikua kazi ya muhimu sana kufanywa na mtu mwenye akili na hadhari kubwa. Ni bahati mbaya sana kwamba CCM mpya haikunisikiliza, leo Cyprian Musiba analia, CCM tunalia. Wote tunalia kwa sababu ya matokeo ya ujinga wa Cyprian.

Ni kama PEPO lilelile limerudi tena ndani ya Serikali ya CCM. Maajabu ya CCM ni kwamba, inafundisha watu halafu haiwatumii. Inatumia watu isiowafundisha halafu wanaharibu. Kosa hili limekuwa likiendelea kila kukicha bila kukoma. Well, unaweza ukauliza; inawezekanaje CCM ifundishe watu halafu isiwatumie itumie isiowafundisha? Jibu ni rahisi, mtu aliyefundishwa anatumwa ndani ya utaratibu. Ukimtuma kazi yako inaishia hapo, mtu aliyefuzu mafunzo vizuri hafundishwi kazi katikati ya kazi kwa sababu ni rahisi kuharibu kazi. Mtu asiyefundishwa, anatumwa vyovyote hata nje ya utaratibu wa kazi. Hashauri wa kukataa mambo yenye kuweza kuharibu kazi. Bahati mbaya CCM inapenda kutuma watu nje ya utaratibu!!

Kama ilivyokuwa wakati wa Cyprian Musiba wakati huu kazi kubwa za muhimu zimepewa mjinga mwingine. Huyu wa sasa anaitwa Steve Nyerere. Yamkinika, huyu ni mjinga kuliko Cyprian Musiba. Inavyoonekana, Steve Nyerere ametumwa kufanya kazi tatu. MOSI. Kuzuia watu wasifikirie Urais wa 2025, PILI. Kuzuia watu wasifikirie madai ya Katiba mpya na, TATU. Kushawishi watu kuchanja J&J. Kazi zote hizi ni za muhimu lakini zimepewa mtu mjinga, matokeo yake zote zitaharibika na kugeuka sumu.

1. Kazi ya kwanza ya kuzuia watu kufikiria Urais wa 2025 imeharibika tayari. Njia anayoitumia Steve inavunja Katiba ya CCM na Katiba ya nchi. Kusema anawaonya watu wenye kufikiria Urais katika CCM ni sawa na kusema kuwa anawaonya watu kufikiria kutumia HAKI yao ya msingi ndani ya CCM, kuchagua na kuchaguliwa. Watu wenye akili watampuuza, watamcheka halafu wataongeza speed.

Kama hiyo haitoshi, Steve amepiga marufuku watu wa CCM kufikiria kuanzisha Chama kingine cha Siasa. Huu ujinga hata Msajili wa Vyama vya Siasa hawezi kuufanya. Hii ndio hasara ya kuwatumia watu wajinga katika mambo makubwa. Kwa kifupi, kauli za Steve zikiendelea zinakwenda kuigawa CCM kabla ya mwaka 2025. Steve haelewi hali ya CCM ilivyo kwa sasa!!

2. Kuhusu Katiba mpya nadhani sipaswi kuongea zaidi. Watu wenye akili hawawezi kumsikiliza mtu mwenye kupinga madai ya Katiba mpya bila kuwapa sababu. Sababu anayoitumia Steve ya kujenga uchumi haina maana yoyote. Uchumi wa nchi sio sababu ya wenye madai ya Katiba mpya. Mtu ana madai yake na wewe unampatia madai yako wapi na wapi? Kwa vyovyote hawezi kukusikiliza. Steve awaambie udhaifu wa madai yao ya Katiba mpya, hiyo ndio hoja yao. Ni bahati mbaya kwamba uwezo huo hana na hawezi kuupata. Hii ndio hasara ya kutuma vilaza kwenye mambo makubwa na muhimu.

3. Kuhusu CHANJO. Nchi yetu imebarikiwa kuwa na Mawaziri wajinga-wajinga sana. Mawaziri wetu hawawezi kutofautisha mambo ya umaarufu na utaalam. Waziri mmoja kwa ujinga wake aliwateua Hamisa Mobeto, Mbwana Samatta na Eddo Kumwembe kuwa mabalozi wa elimu ya KODI nchini. Kwamba watu wasiofahamu lolote kuhusu kodi wakafundishe watu umuhimu wa kulipa kodi. Ni miezi miwili sasa mabalozi hawajulikani waliko na kodi inakwepwa kama kawaida.

Ujinga huohuo umehamishiwa kwenye jambo la Afya za watu. Unamtuma Steve Nyerere anishawishi MIMI kuchanja J&J wakati hana elimu yoyote ya utabibu. Mimi nisiyetaka kuchanja kwa sababu sijafahamu uhakika wa usalama wa J&J kwa miaka mitano au kumi ijayo kwa kuwa hakuna utafiti wa kutosha Steve atawezaje kunishawishi Mimi nisiyetaka kuchanja kwa sababu Serikali haitaki kubeba mzigo wa matokeo ya chanjo kwangu Steve anawezaje kunishawishi nichanje? Nadhani huu ni mzaha katika afya za watu. Kuna tofauti kubwa kati ya kushawishi watu na kuchekesha watu. Watu walioshindwa kumuelewa Waziri wa Afya na Naibu wake ambao ni wataalam wa afya hawawezi kumuelewa mtu mwenye kashfa ya kula rambirambi katika misiba.

Mambo makubwa ya muhimu namna hii katika nchi yote yanakwenda kuanguka kwa sababu amepatiwa mtu mjinga kuyawezesha. Matokeo yake vita ya Urais itakolea ndani ya CCM kwa kauli za Steve, madai ya Katiba mpya yataendelea na yatapanda thamani zaidi kwa sababu ya kauli za akina Steve na CHANJO itakosa wateja kabisa kwa sababu ya ujinga wa Steve Nyerere. Badala ya kushawishi watu yeye anafarakanisha watu. CCM ikiendelea kuwatumia watu wajinga katika mambo makubwa na muhimu namna hii, ijiandae kuanguka katika kila jambo. Ushauri wangu, Steve Nyerere, Kihongos na wenzao wapewe mambo yenye kulingana na vimo vyao. Majuto ni mjukuu!!

Ameandika
MenukaJr
#FikraHuru.
 
Kuna ushahidi kwamba chanjo za COVID-19 zinaharibu seli za damu. Masharti ya chanjo kutokuzingatiwa matokeo yake hayatamalaki

1. Chanjo imeletwa na SSH
2. CCM hoyeee!
3. Samia hoyeee!

Bila kuzingatia vigezo huku mlango wa nyuma wao walipata Pfizer iko tenge.

Same people ndiyo waongeza kodi na tozo.

Kuna mambo hayako sawa na haipendezi.
 
Back
Top Bottom