Serikali ya CCM ina Waziri Mmoja tu.

The Worshiper

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
302
89
“Ni afadhari anayethubutu na kuanguka mara kumi na kuwaumiza watu mara mia kuliko yule asiyethubutu hata mara moja,kwani huyu atawaumiza watu milele”.Ndivyo unavyoweza kuanza namna hiyo kuelezea utendaji wa mawaziri wa CCM.Wengi wamekuwa ni waoga wa kuthubutu na kutoa maamuzi magumu katika masuala mbalimbali ya utendaji wao.Ni rahisi kusikia wakisema pindi wanapokuta madudu kwenye ziara zao wakisema “Mambo haya yamenikera”,lakini baada ya hapo hakuna kinachoendelea.
Kwenye wizara na idara nyingi kuna madudu mengi ,makundi kiutendaji na matukio mengi ya kujirudiarudia(piga picha wizara zote) huku yote yakiwa yanajulikana na wao na hakuna anayethubutu kuchukuwa hatua kali kwa wahusika.Watendaji wengi wa idara na wizara wameshawazoea mawaziri wao na kuwaona ni watu wa kawaida.Kuwazoea huku viongozi wao kunasababisha kucheleweshwa kwa mambo mengi ya msingi ya kimaendeleo na kusababisha mustakabari wa nchi hii kutokueleweka(watu kuumia milele) kwasabababu ya kuwa wazito katika kuthubutu kutoa maamuzi magumu.

Wengi wa mawaziri(wa CCM) wanajifanya wanajua mambo mengi lakini ujuzi huwa haupimwi isipokuwa matokeo na kuwa na ujuzi tu hakusaidii isipokuwa aina ya kazi (uwajibikaji )ndiyo inayoleta utofauti (“It’s not what you know but the kind of job you do that makes difference”). Na hapa ndipo mawaziri wengi unapoweza kuwatofautisha kiutendaji na Mh.John Magufulu.Huyu ndiye waziri pekee wa CCM ambaye yuko makini katika yale anayoyafanya.Ni rahisi kumshuhudia magufuli huku na kule akiwajibika katika wizara yake huku akiwaweka katika wakati mgumu watendaji wavivu na wasiotaka kuwajibika ipasavyo.Kuthubutu huku kwa Magufuli kunawaumiza wachache lakini inakuwa ni neema ya milele kwa taifa.

Mawaziri wa CCM siyo wawajibikaji na hivyo wanashindwa kuwawajibisha waliyo chini yao.Hii ni tofauti na Magufuli.Wanashindwa kuelewa muda walionao ni muhimu tu kwa wakati huo katika kufanya maamuzi (“The time you have is very important at that moment”).Pamoja na wingi wao bado ile kasi inayotarajiwa haionekani hivyo maendeleo ya nchi ni kama ndoto za mchana.Hivyo pamoja na kuwa na baraza la mawaziri kuubwa bado inaonekana (kiutendaji) ni sawa angepewa mtu mmoja na hapa katika wote CCM inaonekana kuwa na waziri mmoja tu Magufuli.


Naomba kuwasilisha!!!
 
"Ni afadhari anayethubutu na kuanguka mara kumi na kuwaumiza watu mara mia kuliko yule asiyethubutu hata mara moja,kwani huyu atawaumiza watu milele".Ndivyo unavyoweza kuanza namna hiyo kuelezea utendaji wa mawaziri wa CCM.Wengi wamekuwa ni waoga wa kuthubutu na kutoa maamuzi magumu katika masuala mbalimbali ya utendaji wao.Ni rahisi kusikia wakisema pindi wanapokuta madudu kwenye ziara zao wakisema "Mambo haya yamenikera",lakini baada ya hapo hakuna kinachoendelea.
Kwenye wizara na idara nyingi kuna madudu mengi ,makundi kiutendaji na matukio mengi ya kujirudiarudia(piga picha wizara zote) huku yote yakiwa yanajulikana na wao na hakuna anayethubutu kuchukuwa hatua kali kwa wahusika.Watendaji wengi wa idara na wizara wameshawazoea mawaziri wao na kuwaona ni watu wa kawaida.Kuwazoea huku viongozi wao kunasababisha kucheleweshwa kwa mambo mengi ya msingi ya kimaendeleo na kusababisha mustakabari wa nchi hii kutokueleweka(watu kuumia milele) kwasabababu ya kuwa wazito katika kuthubutu kutoa maamuzi magumu.

Wengi wa mawaziri(wa CCM) wanajifanya wanajua mambo mengi lakini ujuzi huwa haupimwi isipokuwa matokeo na kuwa na ujuzi tu hakusaidii isipokuwa aina ya kazi (uwajibikaji )ndiyo inayoleta utofauti ("It's not what you know but the kind of job you do that makes difference"). Na hapa ndipo mawaziri wengi unapoweza kuwatofautisha kiutendaji na Mh.John Magufulu.Huyu ndiye waziri pekee wa CCM ambaye yuko makini katika yale anayoyafanya.Ni rahisi kumshuhudia magufuli huku na kule akiwajibika katika wizara yake huku akiwaweka katika wakati mgumu watendaji wavivu na wasiotaka kuwajibika ipasavyo.Kuthubutu huku kwa Magufuli kunawaumiza wachache lakini inakuwa ni neema ya milele kwa taifa.

Mawaziri wa CCM siyo wawajibikaji na hivyo wanashindwa kuwawajibisha waliyo chini yao.Hii ni tofauti na Magufuli.Wanashindwa kuelewa muda walionao ni muhimu tu kwa wakati huo katika kufanya maamuzi ("The time you have is very important at that moment").Pamoja na wingi wao bado ile kasi inayotarajiwa haionekani hivyo maendeleo ya nchi ni kama ndoto za mchana.Hivyo pamoja na kuwa na baraza la mawaziri kuubwa bado inaonekana (kiutendaji) ni sawa angepewa mtu mmoja na hapa katika wote CCM inaonekana kuwa na waziri mmoja tu Magufuli.


Naomba kuwasilisha!!!

Mbona umemuacha waziri wa uchukuzi??
 
CCM wote wameoza!!!! Hata huyo mmoja unayemdhania ni nafuu, ndiye hoi kabisa!
 
Mbona umemuacha waziri wa uchukuzi??
Yule ambaye alinusurika kuuawa na baadaye mafisadi wakamtuliza kwa uwaziri? Kwani unamsikia tena akiwalalaminia wabaya wake? Mbwa mwenye mnofu mdomoni habweki!! Acha tu!!! Rushwa ni kitu mbaya!
 
ok
nilidhani unamsema wanayemigiza akina Ze komedy, aliyeuza kifusi cha madini hivi karibuni
 
Mawaziri wanaotekeleza ahadi za Rais za kupanda udini ni Waziri shekhe Ponda na Waziri shekhe Farid hao ndio wanapiga mzigo kwasababu hawakauki kwenye vyombo vya habari
 
Magufuli ni mpuuzi kama walivyo wengine. Mbona naye ameshiriki kulalamika kuwa maeneo ya mizani wamewajiriwa watoto wa vigogo na wala hajachukua hatua ya kuwataja au kuwachukulia hatua? Kwa nini hakujiuzuru, kama kweli ni mzalendo, ulipopitishwa mpango wa kuuziana nyumba za serikali wakati yeye akiwa waziri mwenye dhamana, na badala yake akamfanyia mipango ndugu yake auziwe nyumba japo hakustahili?

Sema Magufuli anajua kumuigiza Mrema!
 
Maghufuli huyu aliyepiga kampeni za kijinga mpaka mbunge wa Igunga akatenguliwa ubunge, yule aliyewabeza wananchi wa Kigamboni kwamba wapige mbizi kama wanaona nauri kubwa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom