Serikali/Wizara ya Afya Ianzishe Namba za Simu za dharura kwa baadhi ya Magonjwa.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Kuna baadhi ya Watu wanapoteza Maisha au kupata Vilema/Kupooza kwa sababu ya kukosa matibabu ya haraka kwa baadhi ya Magonjwa kama Vile.Pumu,Kiharusi,Shinikizo la Damu,Sukari...nk,Ni vizuri Serikali kushirikiana na W/Afya ingeanzisha namba za dharura kama vile Idara za Zimamoto,Usalama,NK walivyokua na Namba zao za dharura.
Nchi nyingi za wenzetu wao wana hivi Vitengo na Madaktari Spesho ambao wametengwa kwa magonjwa hayo Mfano USA wao wana kanuni yao ya kupambana na Kiharusi/Stroke wanasema FAST...F-Face drop,A-Arm weakness,S-Speech difficult,T-Time for calling...Hapo time for Calling wametoa namba ambazo ukipiga ndani ya dakika chache wanakuja wahudumu wa Afya na kutoa huduma,Wao kuna watu wanaitwa Community drs,family drs hizo ndo kazi zao.
Pia Serikali inaweza kutumia huduma hiyo kupunguza vifo vya mama na mtoto kwani baadhi ya mamawajawazito wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma za haraka hasa maeneo ya vijijini kwani hawajui hata watoe taarifa wapi pindi mama apatapo matatizo.

Ninaimani Serikali yetu kushirikiana na Wizara ya Afya wakijipanga wanaweza kuanzisha Kitengo hiki na kikawa Msaada mkubwa sana kwa Wananchi.
Nawasilisha..
 
Back
Top Bottom