Samahani sana wanajamvi,yawezekana nikawa nimekosea hili ama lile ila kwakuwa mnaelewa mimi ni binadamu bila shaka mtanisamehe. Naenda moja kwa moja kwenye kichwa cha habari yangu, Nina miaka zaidi ya mitatu katika halmashauri ya wilaya Kiteto lakini naona utendaji uliopo wa serikali ya hapa ni sawasawa hakuna serikali kama ifuatavyo.
a.Vipimo katika nafaka- hadi leo hii wanunuzi wa nafaka kama vile mbaazi,mahindi,choroko,alizeti,ulezi nk wananunua kwa ndoo na sio kwa kilo, hii inapunja sana wakulima ila serikali inaangalia tuu.
b.ujazo wa magunia kwa wabebaji (kuli) mahindi yanajazwa hadi kilo 105 kwa gunia wakati katika viwango vya uzito katika ubebaji haipo hiyo hiyo, mashudu ya alizeti yanashindiliwa hadi kilo 110 na kwa uzito huo huo anabebeshwa mtu serikali imaekaa kimya nguvu kazi inaumia tuu.
c.wamiliki wa mashine za kusindika na kusaga nafaka hawatumii kabisa mizani katika kutoa huduma hii, mwananchi anaangaliwa amekujaje anatajiwa tuu kiasi cha pesa cha muonekano wa mzigo hata kama anasaga pumba, basi anabandikwa bei .
02.Huduma za maji. Serikali hadi leo haijaweza kusambaza huduma hii muhimu, ili pindi anapotokea mwananchi kuchimba kisima na kutoa huduma hii bure basi anakatazwa asifanye hivyo inasikitisha sana, mfano wa mwananchi huyo ni Amin H Punja alifanya hivyo na alikatazwa,.
03.Nauli za usafiri.mfano Mbigir-kibaya km 09 nauli tshs 1000/=,Engusero - Kibaya km 29 nauli tshs 3,000/=,Njia panda ya NACO km 96 nauli tshs 10,000/=,Babati- Kiteto km 210 nauli 16,000/=
Nimeweka hapa wanajamvi ili kujaribu kupaza sauti kwenu pengine wananchi HAWA wakatetewa.