Elections 2010 Serikali: Walioachana mswada wa mapitio ya Katiba Zenji Wahuni

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,693
20,453
... Akizungumzia vurugu hizo, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, alisema waliofanya vurugu hizo ni wahuni.

Alisema kikundi hicho cha wahuni kilikwenda katika mkutano huo kwa malengo maalumu, ili ionekane watu hawataki Muungano.

Aidha, alisema amesikitishwa na kitendo cha watu kuchana nakala za muswada huo na kutoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya jazba, lakini alisema maoni yote yaliyotolewa kamati imeyachukua na itayafanyia kazi.

Vurugu hizo zilitokea katika ukumbi wa Shule ya Haile Selassie mjini Zanzibar jana, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, kuchangia kwa maneno makali na baadaye kuuchana hadharani muswada huo na kutoka nje ya ukumbi.

...

Tukio hilo lilisababisha baadhi ya wajumbe kuzichana nakala za muswada huo huku wengine wakinyanyua viti juu wakiashiria kwamba mkutano huo umekwisha na baadhi yao wakimfuata Sheikh Farid nje ya ukumbi wa mkutano.
Tusubiri maimamu watakua upande upi sasa, wa serikali au wa imamu mwenzao! Sitegemei kama watatoa tamko hapa kwani kila upande unawahusu!
 
hahaaaaaaa imamu muhini tena?duuuh kazi mnayo JK na serikali yako
 
Samia, kikwete, na mafisadi wenzao wote ndio wahuni. Haki ni haki bila kujali ni nani anaitetea. Imam alikuwa sahihi kuuchana muswada kwa sababu ni wa kihuni na waliouandaa wote ni wahuni tu.
 
Midraji Ibrahim, Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, amesema vijana waliotaka wabunge wa Zanzibar wajiondoe bungeni ni kundi la wahuni.

Akizungumza kwenye ofisi za Bunge jana, Suluhu alisema vijana hao ni wahuni na kwamba waliamua kufanya hivyo kwa utashi wao na sio kwa utashi wa watu wa Zanzibar.

Suluhu alisema masuala mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa Kamati ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala wakati ikikusanya maoni kuhusu muswada wa kuundwa kwa tume ya marekebisho ya katiba yalikuwa ni mawazo tofauti ya wananchi.

“Wanapokusanyika watu lazima watakuwa na mawazo tofauti, siamini kama kuna Mtanzania hataki amani na usalama wa nchi yetu,” alisema.Alisema kifungu cha tisa katika muswada huo, kinabainisha vitu muhimu kwa taifa ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa kwenye katiba mpya na kwamba wananchi hawakatazwi kujadili jinsi ya kuviboresha.

Kuhusu kero za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi wakati wa serikali ya awamu ya nne, Suluhu alisema wamefanikiwa kuondoa vikwazo kwenye mgawanyo wa mapato.“Serikali ya Zanzibar inapata asilimia 4.5 ya misaada ya kibajeti. Kuanzia mwaka wa fedha 2009/10, SMZ imeanza kunufaika na asilimia 4.5 ya mikopo ya kibajeti,” alisema.

Katika hatua nyingine, Serikali SMZ imeanza kupata misamaha ya fedha ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na kwamba dola 15.12 milioni za Marekani zilitumika kununulia magari, vifaa vya kilimo na vifaa vya Hospitali ya Mnazi Mmoja.

“Imekubalika kuwa SMZ inaweza kukopa ndani na nje ya nchi, chini ya udhamini wa Serikali ya muungano wa Tanzania,” alisema Suluhu.Kuhusu wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili, Waziri huyo alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imetengeneza mfumo mpya wa usawa wa kutathimini Tanzania bara na visiwani na kwamba umeanza kutumika Februari 25, mwaka huu.
 
asilimia 4.5 kwa zanzibar ni kubwa sana ukizingatia uwiano wa idadi ya watu. kama watu 1m wanapata 4.5% na watu 43m wa nchi ileile wanabaki na 95.5% tu, kwa kweli hiyo si haki kabisa

halafu hilo la kudhaminiwa na serikali ya muungano, maana yake nchi ya zanzibar ikikataa kulipa, itailazimu nchi ta tamzania (bara) kubeba mzigo huo! hapa nahisi matope yalichukua nafasi ya ubongo ndani ya vichwa vilivyofikia uamuzi huu. kwa kweli maamuzi kama haya ndiyo yataharakisha kuvunjika kwa muungano huu

mwisho sio sawa kwa waziri kuwaita wote wasiokubaliana na mawazo yake, ya chamachake na ya serikali yake kuwa ni wahuni. hapo anapaswa kuomba radhi kwa wazanzibari wenzake.

huyu mama kama sikosei alichaguliwa kuwemo kwenye CC mpya ya ccm, kwa msingi huu, naamini ccm haijajivua gamba bado
 
asilimia 4.5 kwa zanzibar ni kubwa sana ukizingatia uwiano wa idadi ya watu. kama watu 1m wanapata 4.5% na watu 43m wa nchi ileile wanabaki na 95.5% tu, kwa kweli hiyo si haki kabisa

hawana shukrani kabisa hawa, ni sawa na kumsaidia mtu kisha anakutukana. huu muungano ni product ya cold war, una manufaa kwa wazanzibari kuliko watanganiyika. muungano wa hovyo kuliko yo yote iliyopo duniani.
 
Angesema hayo mwingine tungesikia 'matamko' toka kila kona. Lakini kwa sababu ni 'mwenzetu' kuko kimyaaa! Atueleze 'hao wahuni' ni raia wa wapi.
 
hawana shukrani kabisa hawa, ni sawa na kumsaidia mtu kisha anakutukana. huu muungano ni product ya cold war, una manufaa kwa wazanzibari kuliko watanganiyika. muungano wa hovyo kuliko yo yote iliyopo duniani.

Ndio maana mnatakiwa muijue katiba na mutumie nafasi hii kutoa mawazo yenu ili kuondoa kero na malamiko yenu kuhusu huo Muungano. Kwani pande zote zinalalamika na hilo ni Kosa la JK Nyerere na A Karume ya kupeleka makubaliano kwenye chombo cha kutunga sheria kwa kutumia hati ya dharula na kuupitisha bila kuwapa wananchi nafasi ya kuujadili kwa kina muungano wenyewe.

Zindukeni na toeni mawazo.
 
Kwani Utingo aliekuja na proposal ya Muungano ni Karume au Nyerere? Sasa baada ya kutuvamia kwa miaka 47 na kutudumaza, kudai haki yetu ya kujiamulia mambo yetu imekuwa nongwa?

Tanzania bila Zanzibar haiwezekani lakini Tanzania bila ya Zanzbar haiwezekani.

Daini Tanganyika yenu, wacheni kulala
 
Muhuni ni yeye huyu samia suluhu hassan,analewa,anafanyiwa viLE VILE,muangalieni muslamu gani anatembea kichwa wazi,kwa uwislamu tunakuita wewe muhuni,,,kudadadekiiii

Tuombe radhi tafadhali zako,hapa huru sheik wetu tumeunga nae pia muhuni ? Viongozi wetu pia wahuni ? WEWE Takecare ohooo

Akija zenji ndo anajidai kujifanya kujistiri akija bongo kumbee ndo hivyoo mara unamuona kwa macheniii img_minister.jpg
 
Makosa hapa, ni Serikali zote kuingilia mchakato, kama tunataka amani ni basi swala la muungano serikali ziwe neutral na kuwaachia wananchi kujadili na kuamua. Huyu Samia, tangu lini kaupenda Muungano? ni uongo wa ajabu saana watu tuna detail zake akiukandya akitaka tutashusha
 
I believe the Union btn Tanganyika & Zanzibar has more to do with Communism, Socialism and Capitalism rather than Economical Slavery
 
Huu muungano ni wa kihuni sana, vunjilieni mbali huu muungano, hauna faida yoyote zaidi ya hasara.
 
Kwani Utingo aliekuja na proposal ya Muungano ni Karume au Nyerere? Sasa baada ya kutuvamia kwa miaka 47 na kutudumaza, kudai haki yetu ya kujiamulia mambo yetu imekuwa nongwa?

Tanzania bila Zanzibar haiwezekani lakini Tanzania bila ya Zanzbar haiwezekani.

Daini Tanganyika yenu, wacheni kulala

Kati ya komentz zote hii yako mkuu nimeipenda.
I'm not for the union labda TANGANYIKA nchi yangu itambuliwe ndani ya katiba na kuwepo katiba ya TANGANYIKA kwanza ndo tutunge katiba ya muungano,,, hapa wote wanaoshadadia katiba mpya ya muungano bila kuwepo ya tanganyika mi nawaona wote ni wahuni tuuuuuuu
 
Haya ndio maneno ya kusema Noti mpya na sio kulalamika Zanzibar hivi Zanzibar vile.

Tusikubali kuyumbishwa na kugombanishwa na Viongozi walafi na mafisadi

Daini Tanganyika yenu haraka, sisi ndio tunaanza hivi.
 
Back
Top Bottom