Serikali: Tutawafilisi Mafisadi na Wahujumu Uchumi

for life

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
3,396
4,437
B]
DDP1.jpg

Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga[/B]


Serikali kupitia vyombo vyake vya dola, imetangaza kuzitaifisha mali za wote waliopatikana na hatia ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi na kueleza kuwa utaratibu huo ndio utakaoendelea kwa watuhumiwa ambao bado kesi zao hazijamalizika au hazijapelekwa mahakamani.

Tangazo hilo la serikali limetolewa leo Januari 28, 2016 na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, DPP, Bw. Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi(DCI), Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani na Mkurugenzi wa Upeleelzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wakati wa mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha kuwa jukumu hilo linatekelezwa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai amesema, mwaka 2012 idara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa pamoja walikubaliana kufanya kazi ya ufuatiliaji wa mali zinazohusiana na uhalifu kama sheria inavyotaka na kwa upande wa jeshi hilo tayari kitengo chake cha upelelezi wa makosa ya uhalifu wa kifedha (Money laundering) kiko kazini.

“Katika kutekeleza mkakatihuo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ha hizo ,kesi tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya Mahakama ili ziweze kuzuiwa au kutaifishwa (Restraint or confiscation).” Alifafanua Kamishna Diwani Athumani

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi kutoka TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo, yeye amesema, taasisi yake imeona hakuna maana yoyote kwa mhalifu wa Ufisadi na uhujumu uchumi ukamfunga gerezani na kisha kumuachia baada ya kifungo halafu aendelee kutumia mali alizochuma kwa njia za haramu.

“Tumeona njia mbadala ya kudhibiti hali hiyo na kwa mujibu wa sheria ni kumfilisi mhusika hata kama atatumikia kifungo.” Alibainisha Bw. Alex

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP, Bw. Biswalo Mganga, yeye amesema ili kuendana na dhana ya Hapa Kazi Tu, ni lazima kukabiliana na wahujumu uchumi na Mafisadi ili hatimaye Wananchi walio wengi waweze kunufaika na rasilimali zao.

“Natoa wito kwa nyie waandishi wa habari muujulishe umma wa Watanzania kuwa kama mtu anayo taarifa au anajua mali zinazomilikiwa na mtu isivyo halali hususan watumishi wa umma basi atoe taarifa.” Alisema
 
sawa wambea ndio tunatia timu kuwatumbua wale waliotunyanyasa na pesa za wizi huku wakijua hipo siku tutawatumbua.
 
Kuna mtu ameleta thread ya Ubadhirifu huko halmashauri ya jiji la Mwanza, kwa kuchukulia mikopo watumishi ambao hawapo makazini. Nashauri mwende na huko!
 
Jamani viongozi kuweni WA kweli na haki ya kila Mtanzania ionekane isiwe kwa walala hoi na vigogo wenzenu wanapeta. Sisi yetu macho hatuna la kufanya ila tutasema kwa kukumbushia haya musemayo Leo.
 
Ila wawe wanaweka na namba jamani toka mwaka 2012 ni kesi 23 tu, kati ya hizo 3 tu ndio zimetolewa uamuzi labda wakati mwingine watupe na gharama za kufatilia manake value for money hapa kama tumeuza ng'ombe kufatilia kesi ya kuku. Uzoefu unaonyesha dili moja linapigwa na watu Zaidi ya 5. Ukihesabu dili toka muda huo mpaka sasa ilitakiwa watu kama 230 wawe behind bar na 30 ndio wameshakula mvua na kufilisiwa.

Seriuos jamaa bado sana kama safari ya Mwanza kwa basi ndio wanafika ubungo mataa. Kwa mfano watu wamepiga Zaidi ya container 2,000 tu, acha radar, vitambulisho vya taifa, ujenzi n.k Na hao 3 wangekwambia ni Yona, Mramba na katibu wao.
 
Naye Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP, Bw. Biswalo Mganga, yeye amesema ili kuendana na dhana ya Hapa Kazi Tu, ni lazima kukabiliana na wahujumu uchumi na Mafisadi ili hatimaye Wananchi walio wengi waweze kunufaika na rasilimali zao.

Naona dalili za kuchomoa .............. kuna majipu hayatumbuki. Magufuli hakujua hilo ............ sasa hili la kukubaliana na Mafisadi linatoka wapi tena!!?
 
Tunasubiri kukamatwa kwa Singasinga la Escrow ili mzidi kutuyumbisha tusahau ya Zenji!
 
Wangeanza na wale wamiliki wa makontena yaliyo toroshwa bandarini maana wengi walijulikana....
 
Nimeamua kusema Chenge na JK.Hayo ndiyo mawazo yangu na wewe unaruhusiwa kusema yako.
Usipende kuacha mlango wazi sababu jirani yako jana aliacha wazi kwani bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi!!!
Taarabu, jf ni kila kitu huwezi kuwa bored.
 
Back
Top Bottom