Serikali tunaomba chombo maalum cha kudhibiti mahari kwani tunanyanyaswa na Wakwe!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Haiwezekani maisha ni magumu, Watu tunahangaika usiku na mchana, tunahudumia pengine kuliko hata uwezo halafu hapo hapo ikitokea umependana na Binti au Mwanamke fulani basi " ukijitusu " tu kwenda kujitambulisha kwa Wazazi wake ( Wakwe ) Wewe ndiyo unafanywa MKOMBOZI WAO WA MAISHA YAO MAGUMU yanayowakabili.

Hawa Wazazi ( Wakwe ) hata hawaulizi unafanya Kazi gani au una Kipato kipi wao ukisema tu unaulizia Mahari kwa Mtoto wao kiwango cha chini sana ambacho utatajiwa ni Tsh 5,000,000/ ( milioni tano ) na wakitaja hiyo Pesa huwa wanakuwa " wakavu " kabisa hawana hata aibu.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania najua sasa mnajitahidi kuanzisha Vyombo mbalimbali vya kudhibiti malipo ya huduma mbalimbali tunaomba pia mmulike na huku kwenye utoaji wa Mahari kwani kiukweli sisi Waowaji " tunateseka " mno na wengi wetu ukitupima stress levels zetu utakuta kimevuka wastani kama siyo kupitiliza kabisa.

Hawa Wazazi ( Wakwe ) wanaopenda " kutukomoa " watatufanya sasa na sisi wakishatutajia tu kiwango kikubwa cha HELA ya Mahari nasi tunawadadavulia mapungufu ya hao Mabinti zao.
Kwa mfano Wakwe zako wakikutajia hiyo Shilingi milioni tano na sisi tunaweza kutaja mapungufu ya Mabinti zao ambayo yataendana na upunguaji wa hiyo mahari ambapo tutawajibu hivi:

Sawa Wakwe zangu hiyo mahari nimeisikia ila na Mimi nasema mapungufu ya Mwanenu huyu ambapo kwanza hajui kupika vizuri na anaunguza sana vyakula, pili si msafi sana na huwa natumia muda mwingi kumsimamia, tatu ni mbea mno na huwa nagombana nae mara kwa mara juu ya hili na bado hajaiacha hii tabia, nne ni mvivu kiasi na hawezi kufanya kazi hadi umsimamie na tano bado kiwango chake cha Elimu ni kidogo sana na itabidi nikishamuoa nimuendeleze hivyo basi kwa haya " mapungufu " yake yote ya msingi naomba nitoe tu Shilingi laki tano ( 500,000/ ).

Tumechoka na tumewachoka sana enyi Wakwe zetu kwani hakika mnafanya maisha yetu sisi Vijana tulioamua kwa dhati kabisa kuachana na kupiga " punyeto " ili tuoe mabinti zenu kuwa magumu. Kama nyie mnazo hizo Shilingi milioni tano mbona hamkumsaidia Binti yenu huyu niliyemkuta " choka mbaya? " au kama nyie mnazo hizo HELA mbona maisha yenu ni magumu na mmechoka?

Wazazi wetu na Wakwe zetu badilikeni na sivyo tutaacha kuwaowa hao Mabinti zenu " wawadodee " mje kujuta.

Naomba kuwasilisha huku nikiwa na maumivu makubwa kabisa moyoni!
 
Sijui kwanini mahari hua ni kikwazo kwa familia nyengine lakini walio na uelewa wanajua khasa kua Mahari ni zawadi kutoka kwa Mume anampa mkewe,sasa hayo mambo yakutajiwa hela zote sijui yanatokea wapi,sisi tulienda kumposea Bro
tukapewa list mpaka tukashanga nilijua kwa wengine tuu lakini list yetu tulipewa mpaka Vitenge tena <WAX> kwa maandiko
nikajiuliza hela zote hizo kwani unamnunua au au unamuoa au harudi tena kwao?
 
kha!!!! milion 5++++?????? wa wapi hao???? waachie kina regnad MENGI!!! kama uwezo hauruhusu,,,
 
Back
Top Bottom