Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Serikali imesema ikishindwa kujenga mitambo ya kuchenjua makinikia itakaribisha wawekezaji kufanikisha mchakato huo.
Msimamo huo umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Juni Mosi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka aliyetaka kujua hatma ya zuio la usafirishaji wa makinikia hayo.
"Lengo la zuio hili ni Serikali kujiridhisha juu ya wasiwasi wa wananchi mkiwamo wabunge ambao mmekuwa amkiuliza maswali mengi.
“Baada ya uhakiki huu na ushauri wa wataalamu tutaona kama Serikali inaweza kujenga mitambo hiyo kwenye maeneo yanayotoa mchanga huo kwa wingi. Ikishindwa, tutakaribisha wawekezaji," amesema Majaliwa.
Tangu Machi 3 Serikali ilizuia usafirishaji wa makinikia na kuunda tume mbili kuchunguza ukweli wa taarifa za kilichomo pamoja na mapato stahiki yanayolipwa serikalini.
Chanzo: Mwananchi