Ni kweli kujiajiri kunalipa na kila mmoja anatamani kufanya hivyo. Ila serikali kwa kuwa ni mwajiri, inatakiwa kuwajali waajiriwa wake. After all, hawa ndio wanaoisaidia serikali kuwahudumia watu wake. Hebu jiulize, kama ingetokea KILA MTU akajiajiri kama wewe ulivyojiajiri, ukienda hospitalini ungehudumiwa na nani? Mwanao angefundishwa na nani kama kila aliyekuwa mwalimu angejiajiri akaacha kazi ya kufundisha?
Tumezoea sana kuwakejeli watumishi wa umma au waajiriwa kwa kuwa wana maisha duni. Lakini ni muhimu tutambue kuwa kama binadamu, kila mmoja anahitaji huduma ambazo hutolewa na watu wengine. Kama kila mtu akijiajiri, maisha hayawezi kwenda. Yeye aliye mwajiri na atimize wajibu wake, na mwajiriwa kadhalika. Isije ikaonekana kama kuajiriwa ni laana.