Serikali tatu ndio imegonga mwamba!

Miunda

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
530
182
Tatizo la zanzibar sio Jecha wala sio Shein , tatizo hasa ni hofu ya serikali tatu, kiufupi ni kubadilika kwa mfumo wa muungano na sio kama wanavyo sema ccm kuwa upinzani zanzibar utavunja muungano.

Jengine hofu ya viongozi walio pita ni kwamba pale mfumo utakapo badilika wanaogopa gharama, gharama ambazo zanzibar itakayo dai kwa kupitia serikali ya muungano, kwa mfano hivi sasa zanzibar inakosa zaidi ya bilioni 70 fedha za misaada zisizo kuwa za kibajeti. Mfano mwengine 4.5 ambayo kila mwaka zanzibar inatakiwa kupata, hupata 1.2 -2 kwa mwaka na zilizo baki huishia kwa viongozi wa ccm wakiwemo wa Jamhuri ya muungano na zanzibar.

Fedha hizo ndio wanazo hakikisha wanalindia maslahi yao, na muungano kwa ujumla.

Jengine hofu ya Rais Mstaafu Mkapa, kwa yale maovu alio fanya zanzibar 2001 January 27. Civilians 60 walipoteza maisha na wengine kuwa vilema.

Ni wakati kwa wapenda Tanzania, Tanganyika na zanzibar kudai haki na uhuru wetu na maamuzi yetu, rasimu ya katiba ya wananchi imepinduliwa na CCM na ndio ingelikuwa muarubaini wa muungano, mafisadi, utawala bora na rasilimali za nchi kuwa salama, hivyo basi ifike siku wananchi na vyama vya siasa vya kuzalendo ku stand strong na fight kuhakikisha maamuzi yetu yanaheshimiwa.

Hili taifa sio la ccm wala Nyerere wala Karume, wala ASp wala TANU, ni taifa la watanzania na kamwe tusikubali kufuata mizimu ilio pita, wakati umebadilika, kama viongozi walio pita walikuwa wanaakili nasi tunazo, na tumesoma.

Wakati wa mabadiliko ni wakati wowote na sio uchaguzi tu Ukawa.

Sorry kwa kuwachosha
 
Mnafiki lazima dhambi imrudie watabana ila mungu akiweka mkono yake lazima mafisi yawe kondoo
 
Back
Top Bottom