B.G TANTAWI
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 496
- 379
Sasa ni wazi kuwa Muundo wa serikali tatu hauepukiki kwa nini?
Tanzania bara siyo Nchi na wala siyo jina lake, Jina halisi ni Tanganyika, kwa vyovyote vile hatuna katiba yetu sisi kama watu wa bara au watanganyika, tunatumia katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo ni Muungano wa nchi Mbili za ZANZIBAR NA TANGANYIKA, lakini cha kushangaza Zanzibar wana Katiba yao, Tanganyika hatuna katiba yetu. Well, ikiwa Rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya sasa itabadilishwa katika kipengele cha Serikali tatu kama inavyopendekezwa na Chama cha mapinduzi na baadhi ya watendaji serikalini italeta matatizo, yapi hayo?
Kutakuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, katiba ya zanzibar na Katiba ya Tanganyika.
Kumbuka kuwa Zanzibar wana katiba yao Tayari Inasimamiwa na kutekelezwa na Serikali Huru ya ZANZIBAR,
Tanganyika hatuna katiba yetu na hivyo ndo tunapigania mchakato uanze wa kuiandika, ikiwa tutakuwa nayo ni dhahiri kuwa itasimamiwa na kutekelezwa na Serikali huru ya Tanganyika.
Je! Katiba ya Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Itasimamiwa na kutekelezwa na nani?
proCCM ni blind, hawajui wafanyalo, unajua tunavyo tetea uwepo serikali tatu hawajui hata kwa nini haswa, na hata hawataki kuuliza what is the reason behind! VIJANA WA CCM WA TANGANYIKA KASOMENI KATIBA YA ZANZIBAR YA 2010! Inagalau mtapata upeo, acheni siasa za kukaririshwa na mababu!Ndugu wana JF, Ndugu wana JF, bila shaka mtakumbuka tambo za Katibu Itikadi na uenezi (CCM) kwamba wameteka mabaraza ya katiba kwa 90% upande wa Tanzania bara.
Lakini pia mtakumbuka malalamiko ya Nape wiki iliyopita akidai, "Warioba haitendei haki CCM" kisa kupendekeza muungano wa mfumo wa shirikisho wenye serikali tatu.
Turudi 2010, CCM walikuwa wapi kuingilia kati mabadiliko ya katiba iliyoitaja Zanzibar kuwa nchi? Kama waliona sawa, kwanini hawataki nchi iliyoungana na Zanzibar ionekane kwa sifa na mfumo, kuna siri gani? Tume ya mabadiliko ya katiba imetaja mambo 7 badala ya 22 yaliyopo sasa yaani Katiba na Mamlaka ya JMT, Ulinzi na usalama wa JMT, Uraia na Uhamiaji,Sarafu na Benki Kuu,Mambo ya Nje,Usajili wa vyama vya siasa na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
HOJA;Upande wa Zanzibar, mambo yasiyo ya muungano yatatekelezwa na SMZ, je upande wa Tanganyika yatatekelezwa na nani?
Na sisi majority hatulipendi hili lidudu muungano, ni viongozi plus walinzi wa nchi hii wakishinikizwa na viongozi, tunataka muishie zenu na tukae kwa amani!Watanganyika endeleeni kupiga soga,huku zanzbr tunafanya matayarisho ya mwisho kuitangaza zanzbr ni nchi huru na haina muungano na nchi yoyote,nadhani hapo watanganyika mtazindukana.
Akina Nape, Mwigulu and the likes wamekaririshwa, hawajui wanafanya nini! Wangejua kitu watakuja kujua kitu wanachotetea bila kujua while is too late!Kasimba G; Ni kweli mkuu, mathalani kuhusu mamlaka ya Ukuu wa nchi ibara ya 33 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema, "kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano (ibara ya 33(1)" na ibara ya 33 (a) inasema, "Rais atakuwa Mkuu wa nchi,Kiongozi wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu". Lakini katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 inamtaja Rais wa Zanzibar kuwa, "Mkuu wa nchi ya Zanzibar na Kamanda Mkuu wa vikosi vya idara maalumu ya vyombo vya ulinzi na usalama Zanzibar" Swali; Dhana ya Rais wa JMT kuwa mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa pande zote za muungano iko wapi?
Na nyie muombe mpate uhuru!Watanganyika mkitaka mpate salama basi ni lazima tanganyika irudi.
Watanganyika endeleeni kupiga soga,huku zanzbr tunafanya matayarisho ya mwisho kuitangaza zanzbr ni nchi huru na haina muungano na nchi yoyote,nadhani hapo watanganyika mtazindukana.