Serikali: Taarifa za Wahisani kujitoa kusaidia Bajeti ya 2016/2017 si za kweli

Kizibao

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,011
552
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

Tamko hilo limetolewa na katibu mkuu wizara ya fedha na mipango Dr Servacius Likwelile kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa hivi karibuni Dar

Taarifa hiyo imefafanua kuwa washirika wa Maendeleo bado wanaendelea na kuisaidia serikali katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa makundi 14 kuisaidia bajeti ya Tanzania sio za kweli. Serikali yatoa tamko kuhusu wahisani kuendelea kuisaidia Tanzania katika bajeti Kuu ya 2016/2017

=========================

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU WAHISANI KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KATIKA BAJETI KUU YA 2016/2017

Tamko hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Washirika wa Maendeleo bado wanaendelea kuisadia Serikali katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa makundi 14 ya kuisaidia bajeti ya Tanzania sio za kweli.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa bado makundi hayo yanaendelea kuisaidia bajeti ya Tanzania ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Washirika wa Maendeleo nane waliahidi kuendelea kusaidia Bajeti Kuu wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ireland, Sweden, na Benki ya Dunia.

Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 baadhi ya Washirika wa Maendeleo wameshathibitisha kusaidia bajeti kuu ya Serikali, Washirika hao ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Denmark, Umoja wa Ulaya pamoja na Benki ya Dunia.

Washirika wengine wa Maendeleo wataendelea kuisaidia Serikali kupitia wa Mfuko wa Pamoja wa Maendeleo na Miradi.

Washirika hao ni pamoja na Ubelgiji, Canada, China, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, India, Italia, Japan, Korea ya Kusini, Norway, Sweden, Uholanzi, Uingereza, Marekani na Uswisi.

Washirika wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia bajeti ya Serikali ni Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, BADEA, Mfuko wa OPEC pamoja na Saudia Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.

Taarifa hiyo ya Dkt. Likwelile imeongeza kuwa, Serikali ya pamoja na washirika wa maendeleo wanaoisaidia Tanzania wako katika mazungumzo juu ya namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hizo.

Serikali imewashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika kupelekea juhudi za kimaendeleo zenye tija kwa wananchi.

=========

The Government of the United Republic of Tanzania would like to clarify a statement which appeared in the Guardian newspaper of 31st March 2016 article and other print and social media titled Magufuli’s government hit by more foreign aid cuts. The Government would like to inform the general public that it isnot true that a group of 14 western development partners have announced withdrawal of their general budget support to Tanzania.

Development partners still support the national budget through three modalities namely General Budget support, basket funds, and direct to project funds. In Financial Year (FY) 2015/16 a total of 8 development partners pledged to provide General Budget Support, these include African Development Bank, Canada, Denmark, European Union, Finland, Ireland, Sweden, and the World Bank.

Meanwhile, as for FY 2016/17, African Development Bank, Denmark, European Union and the World Bank have so far confirmed to provide General Budget Support. However, other Development partners will continue to provide support to the 2016/17 national budget through basket funds and project funds.

These include Belgium, Canada, China, Denmark, Finland, France, Germany, Spain, India, Ireland, Italy, Japan, South Korea, Norway, Sweden, Netherlands, United Kingdom, United States of America and Switzerland. Others are International Multilateral Development Agencies, including the African Development Bank, BADEA, Global Funds, OPEC Fund, Saudi Fund, European Union, United Nations agencies and the World Bank.

Due to the ongoing domestic resources mobilization efforts of the fifth Government, it is anticipated that other Development Partners will also continue with the General Budget Support modality. In this regard, the Government is still in discussion with development partners regarding General Budget Support for FY 2016/17.

Moreover the Government in collaboration with Development Partners is in the process of commissioning a study on how best to improve the development cooperation of Tanzania including the dialogue structure.

The Government would like to thank the Development Partners for their continued support towards the development initiatives of the United Republic of Tanzania.

MINISTRY OF FINANCE AND PLANNING
4Th APRIL 2016.
DAR ES SALAAM
 
Mjinga mjinga mmoja alikuwa anatupigia porojo hapa kuwa makusanyo ya trillion 1.3kwa mwezi yanatutosha
Ukisoma between the lines Likwelile ammeanza kuomba
NCHI YA MATONYA
 
Wananchi wanapewa hope, acheni huu usanii
Report ya mwanzo ambayo waliandika BBC walisema source yake alikuwa huyo katibu Mkuu na watu wakaja hapa ya kuwa siyo kweli kwani muandishi alifahamu vibaya na alikurupuka kupeleka ile taarifa BBC Swahili.. Ni kama kawaida waandishi wa habari wa Tz kabla ya ku analyse habari vizuri yeye akarusha tu. tumesikia tangazo kutoka MCC na serikali ilithibisha ya kuwa ni kweli haikupata msaa.. Je uliwahi kulisikia tangazo kutoka hao wahisani 14? na kumbuka hao hao baadhi ya wahisani wa nchi za Europe walitoa tangazo kuhusu uchaguzi wa Zanzibar.. Je kama waliweza kutoa tangazo lile la uchaguzi kwa nini washindwe kutoa tangazo la kukata misaada? Kama unalo wewe official tangazo kutoka kwa hao wahisani linaloonyesha ya kuwa wamekatisha misaada tuwekee basi
 
Kwa hiyo katibu mkuu wa Wizara ya fedha anapingana na kauli za mawaziri wa fedha na mambo ya nje waliotoa matamko juu ya suala hilo, anataka kutuambia mawaziri waliudanganya umma
 
Kwa hiyo katibu mkuu wa Wizara ya fedha anapingana na kauli za mawaziri wa fedha na mambo ya nje waliotoa matamko juu ya suala hilo, anataka kutuambia mawaziri waliudanganya umma
Waziri wa mambo ya nje ametoa maelezo kuhusu MCC tu...hiyo taarifa ya wizara ya fedha ndiyo huyo muandihi alopeleka habari BBC kakurupuka bila ya kufahamu vizuri kilichozungmzwa
 
Report ya mwanzo ambayo waliandika BBC walisema source yake alikuwa huyo katibu Mkuu na watu wakaja hapa ya kuwa siyo kweli kwani muandishi alifahamu vibaya na alikurupuka kupeleka ile taarifa BBC Swahili.. Ni kama kawaida waandishi wa habari wa Tz kabla ya ku analyse habari vizuri yeye akarusha tu. tumesikia tangazo kutoka MCC na serikali ilithibisha ya kuwa ni kweli haikupata msaa.. Je uliwahi kulisikia tangazo kutoka hao wahisani 14? na kumbuka hao hao baadhi ya wahisani wa nchi za Europe walitoa tangazo kuhusu uchaguzi wa Zanzibar.. Je kama waliweza kutoa tangazo lile la uchaguzi kwa nini washindwe kutoa tangazo la kukata misaada? Kama unalo wewe official tangazo kutoka kwa hao wahisani linaloonyesha ya kuwa wamekatisha misaada tuwekee basi
Kwahiyo wewe unachotaka ni official tangazo siyo uhalisia ?

Tuwe wakweli tuache kudanganyadanganya wananchi.
Tumenyimwa misaada, sasa tutatokaje hapa tulipo.
Tufanyeje?
 
Kwahiyo wewe unachotaka ni official tangazo siyo uhalisia ?

Tuwe wakweli tuache kudanganyadanganya wananchi.
Tumenyimwa misaada, sasa tutatokaje hapa tulipo.
Tufanyeje?
Nipe Ushahidi kama tumenyima misaada
Accept that propaganda zenu ukawa zimeenda mrama..
Ili nikuamini maeno yako lazima uje na official statement ya so called 14 members ya wachangiaji kama ilivyokuja ya MCC..
 
Nipe Ushahidi kama tumenyima misaada
Accept that propaganda zenu ukawa zimeenda mrama..
Ili nikuamini maeno yako lazima uje na official statement ya so called 14 members ya wachangiaji kama ilivyokuja ya MCC..
Kumbe uko kichama zaidi, sorry kijana.
Niko kitaifa zaidi.
 
Hawana lolote hao hapa ni shamba la bibi lazima WARUDI wasiporudi wataingia wengine kubeba udongo wa malighafi.
 
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imefafanua kuwa Washirika wa Maendeleo bado wanaendelea kuisadia katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa makundi 14 ya kuisaidia bajeti sio za kweli.

Imesisitiza kuwa bado makundi hayo yanaendelea kuisaidia bajeti ya Tanzania, na kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Washirika wa Maendeleo wanane waliahidi kuendelea kusaidia Bajeti Kuu wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ireland, Sweden na Benki ya Dunia.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile, kwa mwaka wa fedha 2016/2017 baadhi ya Washirika wa Maendeleo wameshathibitisha kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali. Aliwataja kuwa ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Denmark, Umoja wa Ulaya pamoja na Benki ya Dunia.

Wengine watakaoendelea kuisaidia Serikali kupitia wa Mfuko wa Pamoja wa Maendeleo na Miradi. Hao ni pamoja na Ubelgiji, Canada, China, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, India, Italia, Japan, Korea Kusini, Norway, Sweden, Uholanzi, Uingereza, Marekani na Uswisi.

Washirika wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia bajeti ya Serikali ni Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, BADEA, Mfuko wa OPEC pamoja na Saudi Arabia, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.

Taarifa hiyo ya Dk Likwelile iliongeza kuwa Serikali ya pamoja na Washirika wa Maendeleo wanaoisaidia Tanzania wako katika mazungumzo juu ya namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hizo.

“Serikali imewashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika kupelekea juhudi za kimaendeleo zenye tija kwa wananchi,” alisema Dk Likwelile.
 
Back
Top Bottom