Serikali sasa kutoa elimu ya mazingira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali sasa kutoa elimu ya mazingira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Serikali imeingia katika mchakato wa kutoa elimu na sheria ya mazingira ili kukuza uchumi pamoja na kupunguza malalamiko ya wawekezaji nchini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Mazingira (NEMC), Boniventure Baya, katika mafunzo ya wadau wa mazingira.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Baya alisema lengo la mafunzo hayo kwa wadau ni kujenga taratibu za kufanyakazi pamoja kwa kugawana majukumu na kuondoa migongano ya ufanyaji kazi za utunzaji mazingira nchini hasa katika jiji la Dar es Salaam.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Kuna muingiliano katika kutatua matatizo ya utunzaji wa mazingira … hali hiyo inasababishwa na sheria za mazingira kuwa hazieleweki, NEMC kazi yake ni kusimamia sheria hizo zinafahamika na kutekelezwa,” alisema Baya.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alisema ili kupata maendeleo ni lazima mazingira yatunzwe.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Rugimbana alisema Jiji la Dar es Salaam ni kubwa na kwamba hali hiyo inasababisha urasimu wa upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya shughuli za uchumi.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Ili kuondokana na umsikini, kuna umuhimu kwa wadau wa kujua majukumu ya msingi ikiwemo kukubaliana kuwa na sheria moja ambayo italeta mabadiliko,” alisema Rugimbana.[/FONT]  CHANZO: NIPASHE
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...