Serikali: Rasimu haitachelewesha Uchaguzi Mkuu 2015


Informer

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Messages
1,332
Likes
3,321
Points
280
Informer

Informer

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2006
1,332 3,321 280
SERIKALI imesema hakuna kipengele chochote katika Rasimu ya Katiba kitakachochelewesha ama kuzuia uchaguzi mkuu wa wabunge na rais mwaka 2015.

Hayo yalibainishwa jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu hatma ya Katiba ya Tanzania Bara, iwapo rasimu hiyo itapitishwa na kukubali ziundwe serikali tatu.

Alisema endapo Aprili 29 mwakani, kipindi kilichopangwa kupata Katiba mpya ya Muungano, wananchi watapendekeza kuwapo kwa Katiba ya Tanzania Bara, ofisi yake itakuwa tayari kutekeleza hilo katika muda uliobaki bila kuathiri uchaguzi mkuu.

“Baada ya kupokea Rasimu, nasi tulikuwa na mtazamo wa kuangalia suala zima la Katiba ya Tanzania Bara hasa kutokana na kuwa Zanzibar tayari wanayo. Wananchi wakitaka hilo tutalifanya ndani ya muda na tunawahakikishia hakuna kitu cha kuchelewesha uchaguzi mkuu,” alisisitiza.

Werema alisema kwa sasa wanasubiri Rais Jakaya Kikwete arejee nchini na kumpa ushauri na mapendekezo yao kuhusu vipengele vya Rasimu hiyo, likiwamo suala la uundwaji wa Katiba ya Tanzania Bara. Kikwete yuko kwenye ziara ya kikazi Japan na Singapore.

“Tumeanza kulishughulikia hili kwa kutoa ushauri na mapendekezo katika vyombo vya uamuzi, kwani baada ya ku kamilika mwakani, ni lazima kuwepo na sheria ya mpito ya kuendesha nchi baada ya muda huo.”

Werema aliongeza: “Sheria ya Mpito itasaidia namna ya kuendesha Serikali, kwa sababu Rasimu hii ni ya Katiba ya Muungano, pia kuna vifungu na sheria ambazo zitatakiwa kufanyiwa kazi, kwa mfano namna ya kuachiana majukumu, namna ya kushughulikia wafanyakazi na mawaziri waliokuwa kwenye Serikali ya Muungano, tutayakamilisha haya bila kuacha ombwe.”

HabariLeo
 
S

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,835
Likes
3
Points
0
S

sokoinei

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,835 3 0
Watasema yote lakini wakumbuke kua cheo ni dhamana,na hawakuzaliwa navyo.2015 ndo mwaka wa uchaguzi na hakuna wa kujifanya anatetea hapo
 
R

ralphjn

Senior Member
Joined
Jun 1, 2012
Messages
169
Likes
1
Points
33
R

ralphjn

Senior Member
Joined Jun 1, 2012
169 1 33
Huyu naye kigeugeu.si ndo aliyesema from the begining kuwa katiba iliyopo inatosha ,hakuna umuhimu wa katiba mpya.Sasa anachojipendekeza nini?Watasema yote lakini wakumbuke kua cheo ni dhamana,na hawakuzaliwa navyo.2015 ndo mwaka wa uchaguzi na hakuna wa kujifanya anatetea hapo
 

Forum statistics

Threads 1,274,218
Members 490,631
Posts 30,505,044