Serikali Okoeni Watanzania

Mukundumbusya

Senior Member
Aug 11, 2016
165
250
Habari zenu ndugu watanzania wenzangu, poleni na kazi nzito ya kujenga taifa letu, tena kwa sasa kazi ni nzito kweli kweli.
Tarehe 15 December 2016 nilikuta na tangazo la kazi kwenye mtandao huu wa Jamii Forums. Tanvazo hilo liliandikwa na mtu anajiita MUNGU SI MWANADAMU. Katika Tangazo hilo alibainisha kuwa kampuni la Azam linahitaji wafanya kazi huku akitoa maelezo jinsi ya kupata kazi hiyo.
Alielekeza watu kutuma sms 'KAZI kiwandani' na kwamba yeye angejibu baada ya kupata sms na kutoa maelekezo ya jinsi kupata kazi katika kiwanda cha Azam Flour Mills kilichopo Buguruni.
Bila kusita,haraka sana nilimtumia sms 'KAZI VIWANDANI' naye akanijibu kwa kusema 'NIPIGIE'nikampigia. Baada ya salamu na utambulisho akaniuliza 'UNA NGUVU?' nikiamjibu ndiyo.
Akaanza kunipa maelezo, kwenye maelezo yake alinitaka niandae barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa na nionane naye kesho yake saa nne ili anikabidhishe kwa boss, pia alinitaka niambatanishe na Tsh 100,000 kwa ajili ya kumpa boss ili anipe kazi.
Nikakamilisha barua lakini nilipotezea suala la Tsh 100,000. Nikafunga safari na kwenda kukutana naye pale Buguruni, tulipokutana akaanza na story nyingi sana kuhusu maisha yake binafsi ya kujipamba sana kwamba yeye huwa anajitolea sana kusaidia vijana. Katika maelezo yake nikagundua jamaa ni mpigaji/tapeli. Baada ya hapo akaja mzee mmoja toka kiwandani, yeye kwa sauti ya chini akanambia nipe ile 'LAKI' nikamuuliza ya nini? Akanijibu kwa kuhamaki 'KO UNADHANI UTAPATA KAZI BURE?' mimi nikanwambia sina hela yoyote ya kumpa, akaanza kuondoka akielekea barabara ya Mbagala huku nikimfuata kwa nyuma nikimwomba anisaidie.
Nilipoona anakomaa na kudai kuwa namwaribia kazi,nikamwomba anipe barua yangu ili niendelee na mambo mengine. Akaanza kukatalia barua huku akadai 'BARUA ATABAKI NAYO AU TUICHANE' nikamwambia hawezi kubaki nayo wala hakuna barua ya KUCHANWA.
baada ya mvutano wa takiribani dk5 nikamwambia 'MIMI SIWEZI KUTOA HELA ILI NIPATE KAZI HATA SIKU MOJA'alionekana kukata tamaa sana, na akanipa Tsh 200 ili niongezee kwenye nauli nikaipokea na kumshukuru. Kisha akaniacha pale tulipo simama.
Ndugu zangu hiyo ndo hari harisi ya upataji kazi, kama huna mtu wa kukushika mkono basi uwe na hela ya kununulia haki ya kupata ajira.

Baada ya yote hayo nikaamua kujitosa mwenyewe pale kiwandani kuulizia kazi. Mlinzi akanambia kazi zipo, akanieleza kuwa niende kesho yake nikiwa na barua ya utambulisho na Tsh 1000 eti kwa ajili ya usajili.
Kesho yake nilifika pale kiwandani saa 1 asubuhi kama mlinzi alivyonielekeza. Nilikutana na mhusika kama sijajosea jina anaitwa Mzee Gabo. Nikamkabidhi barua pamoja na Tsh 1000 aliyodai eti ni ya usajili. Baada ya hapo akanambia nikanunue nguo za kazi na ninywe chai saa mbili kamili niwe getini. Nilifanya kama alivyonielekeza na saa mbili kamili nikaingia ndani nikiwa na vijana wengine 6 jumla tukikamilisha idadi ya watu 7.
Baada ya hapo tukaungana na kibarua mwenzetu aliyejulikana kwa jina la Amran ambaye alituongoza mpaka kwenye GODOWN ambako tungekuwa tukifanya kazi.
Kazi za kule ndani ni kubeba Mizigo ya kuanzia uzani wa KL 35,50 na 70.
Licha ya kwamba ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya kazi ya namna hiyo, nilifanya kazi kwa bidii sana. Lakini wakati tukiendelea na kazi nikasikia kuwa kazi pale ndani kazi ni 24 hours. Yaani kuanzia ile asubuh ya saa mbili asubuhi mpaka kesho yake saa mbili asubuhi. Kwa kweli nilihamaki kidogo juu ya kufanya kazi 24 hours.
Ilipofika saa 12 jioni nikamfuata msimamizi wetu wa kazi na kumwambia mimi siwezi kukesha na nataka kuondoka. Akasema sawa, akasema apige hesabu ili ajue anapaswa kunilipa shilingi ngapi.
Baada ya hesabu akajua kwamba natakiwa kulipwa Tsh 9600. Kwenye makabdiano ya posho hiyo alitaka kunikata Tsh 500, nilipohoji nakatwa kwa ajili ya nini akanambia muda huu kampuni halijatoa hundi ko ni fedha za mtu binafsi kwa hiyo anahitaji riba. Nikamwambia nitakuja kuchikua kesho kampuni likitoa hundi.
Niluondoka hapo huku nimewaacha vija a wengine wakiwa wametoka nje kutafuta chakula. Kesho yake asubuhi napema nilikuwa tayari nimefika. Nikamfuata mzee Gabo ili nimwombe kama anaweza kunipangia kazi ambayo ntakuwa nafanya kazi kwa masaa 12 tu, akanijibu nimmpe Tsh 5000 la sivyo hana Msaada.
Baada ya kushindikana kutoa hiyo Tsh 5000 nlimwomba anipitishe getini ili nikachukue ile 9600 yangu.
Nlipofika kule ndani nikakuta vijana wanaendelea kufanya kazi, msimamizi akaniambia nijiunge nao ili angalau pesa iongezeke. Nikajiunga nao na tukapiga kazi mpaka 06:51 huku vijana wakiwa wamechoka sana kwa maana walikuwa wamefanya kazi kwa masaa 30 hivi.
Baada ya hapo ulifuata muda wa malipo ambapo mimi nililipwa Tsh 13700 huku kazi ile ya asubuhi nikiwa nimepata Tsh 4100 na kukamilisha Tsh 13700. Kwa upande wa wale ambao wamefanya kazi masaa 30 mfurulizo walikuwa wakilipwa Tsh 9600 ya mchana, 5250 ya usiku na 4100 ya ile asubuhi mpaka saa 7 mchana na kufanya jumla ya Tsh 19850 huku wakikatwa 500 kila mmoja hela ambayo haina maelezo yoyote.

Hitimisho, naomba serikali ijaribu kuangalia mwenendo wa viwanda hivi, kwani mimi naona kumfanyisha mtu kazi kwa masaa 30 ni kumtesa na hiyo kugeuka kuwa mateso badala ya kazi. Pili, ni suala la rushwa. Rushwa imekuwa kama kitu harari kwani kila ukiomba kazi kama huna mtu wa kukushika mkono basi uwe na pesa za kuhongo.
Natambua harakti za nchi kupambana na rushwa kwa hiyo naomba kuwa juhudi zaidi ziongezwe ili kupambana na huyu adui rushwa.
Tatu, hawa vijana ndo taifa la leo, kama watakuwa wanafanyishwa kazi ngumu kiasi kile tena kwa masaa mengi, baada ya muda mrefu ujao hawa vijana watakuwa tegemezi maana miili yao itakuwa imedhoofu pamoja na akili pia kutokana na kutopata muda wa kupumzika.
Ahsante
 

marcs

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
999
2,000
Wewe mwenyewe ulitoa rushwa ya tsh 1000 je c kosa utakemeaje rushwa huku ukitoa rushwa? Kwa nn usibaki nasimamo wa mara ya kwanza?
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
129,224
2,000
Pole sana ndugu Mukundumbusya. Hayo ndiyo maisha hasa kwa mwanaume. Ni kuhangaika. Naamini siku moja baada ya kutoboa utakaa chini na kuwasimulia wanao na wajukuu mapito haya. Kwa work ethic hii uliyonayo naamini utafanikiwa tu.

Sheria za kazi hapa kwetu zinasemaje kuhusu suala hili? Ngoja tusubiri wataalamu waje watudadavulie. Mtu kweli anaweza kufanya kazi masaa 30 mfululizo? Pengine wanajeshi wanapokuwa vitani lakini kwa mtu wa kawaida hata kiafya ni hatari.

Fikisha malalamiko haya pia kwa mamlaka husika na naamini kuwa utasaidiwa. Mungu Akubariki mkuu!
 

marcs

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
999
2,000
Hakuna sheria ya kufanya kazi saa 30 ni kosa vizir kutoa taarifa kwa serikali hatua za kisheria zichukuliwe c kiwanda hicho tu vipo vingi bua tabia hiyo
 

Mukundumbusya

Senior Member
Aug 11, 2016
165
250
Wewe mwenyewe ulitoa rushwa ya tsh 1000 je c kosa utakemeaje rushwa huku ukitoa rushwa? Kwa nn usibaki nasimamo wa mara ya kwanza?
Ni kweli nilifanya kosa. Lakini neno USAJILI lilinichenga kidogo na huku nikisahau kuhoji kuwa ni usajili wa nini. Nilipitiwa kwa kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom