Serikali: Noah ruksa kubeba abiria

Serikali: Noah ruksa kubeba abiria

BashiriOnline

Senior Member
Joined
Nov 5, 2012
Posts
127
Reaction score
44
Naipongeza sana Serikali kwa kuzikubali Noah kupakia Abiria.....
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1368786872099.jpg
    uploadfromtaptalk1368786872099.jpg
    32 KB · Views: 123
  • uploadfromtaptalk1368786896647.jpg
    uploadfromtaptalk1368786896647.jpg
    45.5 KB · Views: 104
  • uploadfromtaptalk1368786937037.jpg
    uploadfromtaptalk1368786937037.jpg
    35.1 KB · Views: 102
Sisi wenye magari ya NOAH tunakupongeza kwa kauli uliyotoa bungeni. Sasa wenye hureeee!!!! tuweke chata ya Mwakyembe kwenye NOAH zetu.
 
Nchi hii bana kila mtu kuvutia kwake hadi nchi itakatika vipande. Eti noah sasa rasmi kama PSV 'Public Service Vehicle'. Sumatra walizikataa kwa sababu za kitaalam, sasa waziri kwa siasa anaruhusu. Tena ametumia ubabe kuruhusu hata zenye makosa mahakamani eti ziachiwe. Viongozi na washikaji wao wengi tayari wanazo hizi gari lakini hizi gari ni ndogo zinafaa tu kwa usafiri binafsi. Kwa mtindo huu msistaajabu kuona hata guta na mikokoteni kuruhusiwa kubeba abiria katika miji na majiji. Badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma, ndio sera ya uchumi 'huria' ya ccm
 
Nakumbuka mjini Tabora kuna wakati katika kutafuta riziki vijana kwa wingi sana walijiingiza kutoa huduma ya kubeba watu kwa baiskeli! Ni usafiri salama sana, wingi wa watoa huduma hii ambayo inawezekana iliwasaidia sana wateja wao ilileta nongwa toka kwa wamiliki wa Taxi baada ya kuona watu wengi hawahangaiki kukodi Taxi, Taxi drivers wakaanzisha vita kutaka kuwaondoa wenye baiskeli hata kuanza kuwagonga, kipindi hicho boda boda ilikuwa haijakolea. Fujo zilipozidi, Mkuu wa Mkoa (kama sijakosea) aliwashauri wamiliki wa Taxi kwamba anaeona biashara ya Taxi sasa hailipi apaki gari lake au basi waingie nao kwenye usafiri huu kipenzi cha wateja!

Huko Misri Jiji la El Arish kwenye jangwa la Sinai lililoko karibu na lango la Rafa kuingia Ukanda wa Gaza, Jiji hilo usafiri maarufu unaohudumia watu ni vigari vya Benzi vyenye shepu kama saloon vyenye uwezo wa kubeba abiria 6 lakini zinafanya biashara kwa kusanya jijini.

Kenya kuna vigari Toyota Probox, zimejaaa kama utitiri zikihudumia watu kama daladala kuwapeleka nje ya jiji. Probox za Kenya huwezi kulinganisha na Noah! Na nilikuwa nashangaa kuona Kenya wanaruhusu Probox wakati Tanzania wamezuia Noah ambazo zinanafasi na uwezo mkubwa kuliko Probox.

Nadhani wale ambao maslahi yao yataathirika kwa kuwepo Noah barabarani watatafuta vizingizio vya kitaalamu au kuwapaka matope wanasiasa, lakini suala ni kwamba nchi zetu hizi zinatatizo kubwa la usafiri! Kuna maeneo mengi watu wanatumia usafiri wa Malori na Landrover 109 mbona hizi hazilalamikiwi?

Wafanya biashara wa NOah Morogoro kwenda Dodoma wamekuwa wakifanyiwa fujo sana na wamiliki wa mabasi (waarabu na wahindi) baada ya kuona kuwa share yao kubwa ya abiria imemegwa na Noah! Kwa vile ni matajiri walifanikiwa kujenga hoja kwa Trafik wa Morogoro matokeo yake ilikuwa inashangaza Mkoani Morogoro Noah zilipigwa marufuku, lakini ukienda Singida, Nzega, Shinyanga na kanda ya Ziwa Michomoko imejaa inahudumia watu.

Tusome alama za nyakati kuelewa soko linataka nini na kuendana na mahitaji ya Soko, waziri Mwakyembe ni Intelligent person na hakika kasoma alama za nyakati. Hayo magari yalitengenezwa kwa matumizi ya abiria na siyo mbuzi, hata kama ni family car bado hao nao ni watu wale wale!
 
Nawe tafuta ya kwako uanze biashara hiyo, kama zinaruhusiwa kuingia nchini, maana yake ziko salama.
 
Noah ni salama sana kwa abilia.Mkubali mkatae
Tena ni salama kuliko hata mabasi aiseee.
 
Mkuu BashiriOnline, tuko pamoja kwa hilo. Usalama wa chombo chochote cha usafiri uko mikononi mwa Dereva! Tatizo siyo aina ya gari bali waendeshaji. Hata coaster miaka ya nyuma safari za Moro Dar zilichinja sana watu hadi wakawa wanakimbilia kupanda mabasi makubwa! Tatizo ilikuwa ni spidi zinazosababishwa na madereva kutaka kupiga ruti nyingi kwa siku! Haya mabasi makubwa yenyewe ndiyo huwa hayapati ajali? Sote tuko Tanzania na tunapata mishituko kila mara juu ya mabasi makubwa yanavyopata ajali mbaya! Huko Mbeya Manispaa (jiji?!) mwaka huu kumetokea ajali nyingi mbaya sana za magari ya daladala Hiace wala chanzo haikuwa aina ya gari!! Hizi kelele zilizoshamiri dhidi ya Noah siyo kutoka kwa abilia bali ni wafanyabiashara ambao wanaathirika na huduma iliyokubalika ya magari ya Noah. Madereva waelimishwe juu ya ubaya wa kukimbiza sana magari haijalishi ni Noah, Hiace au Macopolo!!
 
Back
Top Bottom