1. Nadhani tutakua tunaionea Serikali kwenye hili. Kwa maoni yangu, migogoro imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wafanyakazi wa wizara ambao wamekua sio waaminifu, ambao wamekua wakitoa nyaraka za umiliki mara mbili au zaidi kwa kipande kimoja cha ardhi.
Ingawa pia, siku zinavyozidi kusonga, tuelewe kwamba migogoro ya ardhi itazidi kuongezeka kwa sababu (a) idadi ya watu inaongezeka, lakini ukubwa wa ardhi upo palepale, kwahiyo uhitaji unakua mkubwa, na hilo pekee linaweza pelekea kuwepo kwa migogoro ya ardhi hasa maeneo ambayo yameshakuwa na miundo mbinu, kama barabara, umeme, vyanzo vya maji nk. (b) Migogoro inaongezeka/ itaendelea kuongezeka kwakua siku zinavyosonga uelewa wa watu/ watanzania juu ya thamani ya ardhi pia unaongezeka, jambao ambalo linapelekea watu kuitafuta ardhi kwa gharama kubwa ( kama vile kutumia pesa, na madaraka nk.).
2. Swala la utambuzi wa wamiliki wa ardhi kwa kutumia kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni muelekea mzuri, endapo Serikali itajiridhisha kwamba kila mwenye kitambulisho cha NIDA ni raia wa Tanzania ( maana kuna uwezekano mkubwa raia wa Kenya, na Congo wakawa na kitambulisho hiko). Na pia, Serikali ijihakikishie kwamba kila Mtanzania anayestahili kupewa kitambulisho amepatiwa kitambulisho ili awe na nafasi ya kumiliki ardhi. Sina hakika kama mpaka kufikia July 2021, wananchi wa Kigoma vijijini wanaomiliki ardhi watakuwa wamepatiwa kitambulisho cha NIDA, vinginevyo naliona zoezi hili ni endelevu, kulingana na kasi ya utoaji wa vitambulisho. Hata hivyo, Wizara tayari imeshaweka muongozo
Kiujumla, swala la kitambulisho cha NIDA halikwepeki, huko tuendapo NIDA ndio itatumika katika ofisi zote kama nyaraka KUU ya utambuzi, na ni bora kwa kila mtanzania ambaye hajapata kitambulisho hiko afanye jitihada kukipata.