Serikali na ugonjwa wa malaria

Serikali na ugonjwa wa malaria

Habari za mda huu wadau!

Baada ya salamu niende direct kwenye mada,, Kumekua na changamoto kubwa mahospitalini siku za hivi karibuni haswa katika kipimo cha malaria na upatkanaji wa ugonjwa wenyewe

Nikiwa kama mhanga wa hili jambo niliamua kufanya utafiti wa kwanini malaria imekua ishu kupatikana

Nilichukua jukumu la kupima malaria mara tatu katika hospitali tofauti ila majibu yalikuja NEGATIVE katika hospital zote

Nilimpima mwanangu pia mara mbili kwa nyakati tofauti ila bado hakupatikana na malaria ila dalili zote zilionesha ana malaria. Hapo ndipo nilipoanza kutilia shaka kipimo cha malaria kwani mwanzoni nilkua nalia na vituo vya afya vilivoko mkoani kwetu

Mara ya mwisho kupima malaria mi mwenyewe ilkua wiki iloisha na bado sikupatwa nayo,, nikaamua kumhoji maswali daktari aloniattend

Nilimuuliza kwanini malaria imekua tatizo kupatkana?, yule dokta aliniangalia kwa aibu kisha nae akaniuliza we unahisi kwanini haipatkani, je imeisha??

Nikamjibu sidhani coz hakuna kilchobadilika katika mazingira tunayoishi

Ndipo alipotoa povu lake kwenye vipimo vya MRDT kwa kusema serikali imelazimisha kipimo cha MRDT kitumike badala ya microscope, MRDT haitoi majibu sahihi ya malaria na haina uwezo wa kuona malaria kidogo mpaka malaria nyingi, na serikali inafanya hivo ili kuhadaa wafadhili watoa vyandarua kuwa malaria imepungua kama sio kuisha nchini ili misaada izidi kumiminika

Jamani! kwaiyo serikali ya wanyonge imeamua raia wake tufe ili kuwafurahisha mabwana wakubwa??

Kuna manufaa gani kwenye hio mrdt nauku haitoi matokeo chanya?? tuhurumieni wanyonge, nyie mkiugua mnakimbilia nje sie ni wa hapa hapa, tendeni haki na mseme ukweli mrdt ni sanaa

Wataalamu wa vipimo ndio wanazingua na sio kipimo mkuu. Usije danganyika tena.
Vitu watu wanavyokosea ni"
*uhifadhi mbovu wa vipimo, mRDT zikihifadhiwa katika mazingira yasiyo rafiki zinapoteza ubora.
* vipimo kuexpire, hilo nimeina sehemu nyingi either ile strip au buffer unakuta imepitwa na wakati na watu wanatumia tu kama kwamba hawaoni.
* mazoea, wapimaji wengi wanatumia uzoefu badala ya kufuata SOP.
*ulr mtindo wa kuchanganya changanya buffer sijui kwa nini watu hawauachi, wataalamu strips zikiisha na yale maji katupe tu, sasa kuna wengine wanayahifadhi miezi na miezi kwa nini usipate majibu ya uongo.

mRDT iko very sensitive, shida ni sisi. Japo binafsi kucheki malaria huwa naenda kwa BS ni kea vile tu nakuwa na uhakika na mtu anayepima au ikibidi nasimamia shoo mwenyewe. Bs for MPs inapoteza muda, na ni rahisi mtu kutoa majibu ya uongo kwa kutokujua au kuona vibaya au kuwa na haraka. Serikali iweke mkazo tu kwa mafundi sanifu wa maabara kuwa makini na hizo mRDT bado zinatufaa sana.
 
Uko mbali sana na uhalisia, utakua unaishi zama za ujima

Ukibainika na serikali unatumia microscope utajuta kuzaliwa tz

Sa we hizo sera za kutumia microscope na mrdt kwa pamoja sijui umetoa wapi
Acha upotoshaji...sasa kuna Sera ya maralia microscope na serekali inafundisha wataalamu nchi nzima,hii ni ili kujua parasitemia/quantity and speciation tofauti na mrdt,pia serekali inagawa darubini Kwa waliowafundisha..kama hujui kitu better kunyamaza
 
Wataalamu wa vipimo ndio wanazingua na sio kipimo mkuu. Usije danganyika tena.
Vitu watu wanavyokosea ni"
*uhifadhi mbovu wa vipimo, mRDT zikihifadhiwa katika mazingira yasiyo rafiki zinapoteza ubora.
* vipimo kuexpire, hilo nimeina sehemu nyingi either ile strip au buffer unakuta imepitwa na wakati na watu wanatumia tu kama kwamba hawaoni.
* mazoea, wapimaji wengi wanatumia uzoefu badala ya kufuata SOP.
*ulr mtindo wa kuchanganya changanya buffer sijui kwa nini watu hawauachi, wataalamu strips zikiisha na yale maji katupe tu, sasa kuna wengine wanayahifadhi miezi na miezi kwa nini usipate majibu ya uongo.

mRDT iko very sensitive, shida ni sisi. Japo binafsi kucheki malaria huwa naenda kwa BS ni kea vile tu nakuwa na uhakika na mtu anayepima au ikibidi nasimamia shoo mwenyewe. Bs for MPs inapoteza muda, na ni rahisi mtu kutoa majibu ya uongo kwa kutokujua au kuona vibaya au kuwa na haraka. Serikali iweke mkazo tu kwa mafundi sanifu wa maabara kuwa makini na hizo mRDT bado zinatufaa sana.
Uko sahh lakn izo sababu zako sio za kweli nenda kasome tena couses of false negative kwa manual ya MRDT.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom