abdulrahim
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 408
- 286
Habari Ndg!
Kwa miaka mingi nimekuwa mkereketwa wa mfumo wa elimu nchini Tanzania. Miaka ya hivi karibuni namba ya school drop imekuwa ikiongezeka kwa kasi saana na bado sijaona mfumo rasmi unaowekwa baina ya serikali na jamii kwa ujumla katika kuwatambua kundi hili.
Kwa ngazi ya familia imekuwa ikiwapeleka vijana wake wanao fail kuendelea na elimu ya sekondari kwenye vyuo vya ufundi zaidi na uuguzi kwa kiasi fulani. Matokeo yake vijana hawa wanafudhu na kuwa mafundi hodari na wauguzi hodari lakini wakija kwenye soko la ajira wanakutana na swala la kuhitajika cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari na kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia kwamba kada hizi ndizo zilizoongoza kwenye wimbi la wenye vyeti feki.
Ombi langu kwa serikali, Nazani sasa ni wakati muafaka wa kuandaa mfumo rasmi wa kuendeleza wale wote ambao ni STD V and Form IV failure kupata taaluma mbalimbali ambazo baadae zitoe fursa za wao kupata ajira za ndani ya nchi na nje ya nchi pasipo hitajika vyeti vyao vya elimu ya sekondari (NECTA certification)
Leo asubuhi wakati naangalia TBC1 niliona mbunge wa CUF Pemba akiongelea sekta ya utalii na mali asili. Kwenye mazungumzo yake alitolea mfano wa India ilivyofanikiwa kuwarasimisha vijana wake wanaoshindwa kuendelea na mfumo rasmi wa elimu(formal sec and Collage education) kwenye kada mbali mbali kama; Ufundi wa kuzibua vyoo, Uunganishwaji wa mabomba ya mafuta na maji, Utumishi wa mahotelini na majumbani.
Nchini India kijana anayeshindwa kuendelea na masomo, Moja kwa moja anapelekwa kwenda kushiriki kwenye kazi za vitendo e.g Ujenzi na baada ya miaka miwili ama mitatu amewekewa msingi wa kurudi darasani na baadae kurudi tena kazini na hatua ya mwisho kurudi tena darasani na kuhitimu.
Kwa njia hii india imefanikiwa kuteka ajira nazani duniani kote na ndio maana kwenye kila kada sehemu yoyote duniani imekuwa sio kitu kigeni tena kukutana na Mhindi.
Huu ni wakati sasa wa serikali kujifunza namna mbali mbali za kuokoa kundi hili na hali hii isibothibitiwa basi wimbi la wataalamu wasio na sifa (Fake Professionals) litakuwa likiongezeka kila kukicha.
Mfano mdogo tuu; Dereva wa Halmashauri ana ulazima wa kuwa na cheti cha kidato cha nne ili apatiwe kazi kweli? Nazani kujua kuongea kwa ufasha lugha ya Kiswahili na kingereza pamoja na kuwa na mafunzo ya magari na udereva ingetosha kumpatia ajira rasmi kijana huyu wa kitanzania.
Hali kadhalika kwa walinzi, Watunza kumbukumbu, Wauguzi n.k!
Naomba kuwasilisha!!!