Serikali na afya za wananchi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na afya za wananchi wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chona, Jan 30, 2012.

 1. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Siku zote nimekuwa nikihamini kuwa serikali yetu haina uthubutu na wala jitihada za kumsaidia mtu wa chini (watu wasiokuwa na uwezo/ watu wa hali ya chini).
  Katika kuthibitisha hilo jana waziri mkuu Mizengo Pinda aliutangazia umma na hasa Madaktari waliogoma kushinikiza kutafutiwa ufumbuzi kwa madai yao kuwa, KAMA HAWATA REPORT KAZINI basi serikali itaviagiza vikosi vyake vya JKT kuwahudumia wagonjwa.

  Swali linakuja kuwa iwapo serikali inajua kuwa kuna vijana wengi walioko JKT wenye uwezo wa kuhudumu kama madaktari kwanini haikuwapeleka mapema mahospitaini ili kunusuru roho za watu zilizopotea katika danadana hii ya serikali na madaktari? Kwanini tusubili watu wengi wapoteze maisha ili hali tunao watu wenye kuweza kusaidia. Ni mara ngapi serikali imesikika ikijitetea kuwa na ni ukweli usio pingika kuwa uwiano wa wahudumu wa afya na hasa madaktari na wananchi wa kawaida ni mdogo. Sasa hao wa JKT wametoka wapi au ni kwamba wao wapo huko wamekaa tu kusubilia dharura.
  Serikali iache siasa kwenye mambo ya msingi iwapo inahitaji kuvusha taifa hili kutoka hapa tulipo kwenda hatua nyingine. Tunahitaji kuona suala hili likiisha kwa pande zote kukubaliana na wala sio kutishana. Kwani wakienda kazini kisha wasihudumie kwa moyo nani wa kulaumiwa. Au kwa vile viongozi wao wananafasi ya kuhudumiwa na hospitali, au daktari wanyemtaka na hata kwenda nje ya nchi. Wananchi waamuke wajue ni nani mchawi wao. Kwa jinsi ninavyoona mchawi wa huduma za afya ni serikali nyenyewe.
   
Loading...