Cobra70
JF-Expert Member
- Jan 2, 2020
- 248
- 550
Mimi nawaza hivi taasisi nyeti za serikali kuna watu wameziua kimaksudi kwa kuajiri watu kiundugu au kwa utashi wa kisiasa! Pia napata shaka mamlaka ya vetting hivi kweli nchi hii hatuna watu SMART na wazelendo kwelikweli?
Kwa sasa nahisi wahuni na watu janjajanja nyingi wanafanikiwa kupenya kwenye taasisi mbalimbali na wenye uwezo na weledi kufa na vipaji na maono yao.
Kwa sasa vijana wengi wanaonekana kutokuwa na maadili kulingana na miiko ya kazi zao mfano unakuta baadhi ya watu. Wao wanashirikiana na watia nia ya ubunge katika harakati za kusambaza rushwa kwa wajumbe badala ya kuzuia au kuwapin wao ndio wanakuwa watonyaji kwa wabunge watoa rushwa na hivyo kuzalisha taifa la viongozi ambao hawana maadili na wasiowajibika kwa wananchi.
Naiomba serikali na hasa chama cha kikuu tawala muviimarishe vyombo vya ulinzi na usalama kwa wakati huu hali ni tete mtaani rushwa imetamalaki.
Tusiruhusu ili suala kutokea mana kwenye kura za maoni watapita wabunge wenye ukwasi ila wasiopendwa na wala kuwajibika kwa wananchi na iwapo uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki na CHADEMA wataruhusiwa kuweka wagombea chama kikuu kina dalili kubwa na wala pasipo shaka kupoteza idadi kuwa ya wabunge na madiwani.
Kwa kumalizia chama kikuu tawala nakishauri kiruhusu wanachama wote wenye kadi na waliosajiliwa kielectroni wapige kura za maoni kuchagua wabunge na madiwani ili tuweze kupata viongozi walio bora, wachapa kazi, wenye maadili na wanaowajibika kwa wananchi na si kuwaachia wajumbe tu wanaoongeka kirahisi.