figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,859
Serikali yasema imeanza mchakato wa kununua meli mpya itakayotoa huduma ndani ya ziwa Victoria.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi katika mkoa wa Kagera kuwa serikali tayari imeshaanza mchakato wa ununuzi wa meli mpya na ya kisasa itakayotoa huduma ya usafiri ndani ya ziwa Victoria kati ya bandari ya Bukoba na Mwanza ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba idadi kubwa ya abiria pamoja na mizigo yenye uzito wa tani 300 kwa wakati mmoja.
Waziri huyo aliyemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa wa Kagera ameyasema hayo baada ya kutembelea bandari ya Bukoba, amesema meli mpya itayonunuliwa itakuwa na uwezo wa kutumia masaa machache ya kusafiri toka bandari ya Bukoba hadi bandari ya Mwanza tofauti na muda ambao ulikuwa ukitumiwa na meli za MV. Victoria na MV. Serengeti zilizokuwa zikitoa huduma ya usafiri katika bandari hizo.
Amezungumzia mambo yaliyokuwa yakikwamisha mchakato wa ununuzi wa meli hiyo ni pamoja na kukosa wazabuni wenye sifa, hivyo akasema serikali katika kuharakisha mchakato huo imebuni mpango mpya kumpata mkandarasi mwenye sifa.
Nao baadhi ya wadau wa bandari ya Bukoba wakizungumza kwa nyakati tofauti kufuatia ziara ya waziri huyo katika bandari hiyo wamesema hatua iliyochukuliwa na serikali ya kusimamisha meli zilizokuwa zikitoa huduma ya usafiri katika bandari hiyo kuwa imeaathiri sana hivyo wakaomba ununuzi wa meli mpya ufanyike haraka.
Chanzo: ITV