Serikali kuwasilisha bungeni sheria mpya ya mikataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kuwasilisha bungeni sheria mpya ya mikataba

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Warema  Serikali inatarajiwa kuwasilisha katika Bunge lijalo sheria inayosimamia mikataba ambapo watu binafsi wataweza kuingia katika utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo ya ujenzi kama wa barabara, viwanja vya ndege na bandari.
  Hayo yameelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Warema wakati anafunga mafunzo ya usimamizi wa mikataba mikubwa ya ujenzi kati ya sekta ya umma na sekta binafsi mjini hapa.
  Jaji Warema alisema kupitia sheria hiyo sekta binafsi itaweza kuingia mkataba na serikali baada ya kufanyika kwa upembuzi yakinifu katika kujenga mradi wowote ule na baada ya kukamilika utasimamiwa na watu binafsi ili kurudisha gharama za ujenzi.
  Alitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na ile ambayo inaangukia katika huduma za kijamii, shule na hospitali.
  Alisema kuwa mtu binafsi kampuni ama kikundi kitaweza kutathimini mradi na baadaye kuingia mkataba na serikali ama taasisi yake yoyote ili kuhakikisha mradi unatekelezwa na baadaye pande zote kupata faida.
  “Tunataka kuondoka katika mazoea kwamba kila unaposikia barabara imejengwa basi lazima kazi hiyo ifanywe na Wakala wa Barabara nchini-(Tanroads) ama Halmashauri za Wilaya,” alisema.
  Warema alisema serikali imekuwa ikibuni miradi mingi na kuandaa michoro lakini imekuwa ikikwama katika utekelezaji wake kutokana na ukosefu wa fedha kazi ambayo ingeweza kufanywa na sekta binafsi.
  Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mradi wa kanda ya Afrika wa kuzijengea uwezo taasisi za serikali katika kuingia mikataba ya miradi ulioko chini ya Shirika la Mandeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), yamewashirikisha wanasheria kutoka katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wanasheria kutoka wizara mbalimbali.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...