Serikali kuwalipa wanachama wa DECI mabilioni yao

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
60,412
Reaction score
88,727
Umofia Kwenu wana JF,

Serikali ipo kwenye mchakato wa kuwalipa wanachama wa DECI takribani bilioni 19 za wanachama wake.

»Haya, mliopanda mbegu kaeni mkao wa kula kurudishiwa mishiko yenu.

Serikali imesema kuwa inafanya utaratibu wa kuwalipa fedha takribani Sh. bilioni 19 za waliokuwa wanachama wa Taasisi ya Development Entrepreneurship Community Initiative (Deci).

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alisema fedha hizo zimehifadhiwa katika akaunti ya Benki Kuu (BoT) na kwamba kinachofanyika sasa ni uangalizi wa kiasi cha michango iliyochangwa na wanachama ili waweze kulipwa kwa usahihi.

"Bado fedha zinashikiliwa BoT uchambuzi unaendelea kufanywa kwa umakini wa hali ya juu, utakapokamilika wanachama wote waliochanga fedha watalipwa," alisema Mkuya.

Aidha, Waziri Mkuya alisema siyo jambo litakaloweza kuchukua muda mfupi kukamilisha mchakato wa malipo ya wanachama hao, kwani linahitaji muda wa kutosha kufanyiwa kazi kikamilifu, ingawa hakutaja kiasi kilichopo.

Mwaka 2009 serikali ilisitisha shughuli za Deci na kuwafungulia mashtaka wakurugenzi watano wa taasisi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na Agosti 19, mwaka 2013, walihukumiwa.

CHANZO:
NIPASHE

Yan hawa jamaaa wa serikali kila ktu wanatake easy ingekuwa wao ndo wanadai fasta kitu kingesoma ndan ya dakka
 
Danganya toto hiyo, huu mwaka tutasikia mengi sana, ni sawa na pale mwanaume anamtongoza mwanamke, kila kitu ataahidi, akipata tu huyo humuoni ndio haya,. wakishawahadaa, wakapata kura watakuja na mala leteni risiti zenu tuzihakiki!! ndio zengwe nitaanzia hapo hapo, uhakiki uhakiki, uhakiki!!!
 
Changa hilo, yaani pesa wale wachungaji eti serikali ije ilipe thubutuuu, ingekuwa serikali kweli ingeliwalipa kwanza walimu wanaodai miaka, mwaka huu tutadanganywa sana.
 
Mkuu kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba serikali ili-freeze account ya DECI na kuzichukua fedha zote na kuzihifadhi BoT na ikawafungulia kesi wakurugenzi wa DECI wale wachungaji.
 
Wakati serikali inataifisha account ya deci ilikuwa na 1bilion tu, Leo inataka Leo inataka kulipa b 19 zimetoka wapi pesa?
 
Hata kama watawarudishia watu fedha zao kweli.....Cha kujiuliza ni wangapi wana receipt?
 
Pyramid schemes is an offence in tanzania hivyo basi hao watu hawapaswi kufaidi matunda ya uovu wao kwanza inabidi washitakiwe kwa kushiriki kwao kwenye dec
 
Pamoja na kufulia kote kwa serikali ya ccm mnaamini kweli hizo hela zitarudi, rejea EPA ESCROW na deep green. Hizi ndio zile tunaambiwaga sio za uma wakati zipo mikononi mwa uma.
 
du naendelea kuzitunza lisit zangu maana niliweka zaidi ya milioni moja. Du hiyo itakua afadhali
 
Ngoja nianze kutafuta risit zangu nilizopandia mbegu juu ya mawe,
 
Mkuu kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba serikali ili-freeze account ya DECI na kuzichukua fedha zote na "KUZIHIFADHI" BoT na ikawafungulia kesi wakurugenzi wa DECI wale wachungaji.

Mkuu hapo nilipoweka herufi kubwa panahusu.
 
Back
Top Bottom